loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tarura yahitaji bil 827/- kuboresha barabara za jiji

WAKALA wa Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA) inahitaji takribani Sh bilioni 826.9 kutekeleza mpango wa muda mrefu wa kuziboresha barabara mbalimbali katika mitaa ya jiji la Dodoma ili ziwe bora, imara na zipitike kwa urahisi wakati wote.

Akizungumza jana, Mratibu wa Tarura Mkoa wa Dodoma, Lusako Kilembe alisema fedha hizo zitahusisha kuboresha barabara zenye urefu wa takribani kilometa 472.44.

Kilembe alisema kwa kuboresha barabara hizo ambazo zinaharibika kutokana na magari kuongezeka, hivyo ili kupunguza pia msongamano kati ya jiji inatakiwa kuboresha barabara za pembezoni ili kupitika kwa urahisi.

Alisema uboreshaji wa barabara hizo za jijini utahusisha barabara ya Makole yenye urefu wa kilometa sita kwa gharama ya Sh bilioni 7.6 na uboreshaji barabara ya Iringa katika eneo la Michese-Chididimo na kujenga makaravati Michese umbali wa kilometa 14.10 kwa gharama ya Sh bilioni 16.4.

Pia utahusisha uboreshaji wa barabara ya kijamii ya Miganga yenye urefu wa kilometa 30.45 kwa gharama ya Sh bilioni 38.14 na barabara ya jamii ya Mkonze yenye urefu wa kilometa 15.35 kwa gharama ya Sh bilioni 19.9 pamoja na barabara ya Ndachi yenye urefu wa kilometa 30.01 kwa gharama ya Sh bilioni 38.8.

Pia utahusisha kuboresha barabara ya Mwangaza-Kisasa-Medelii yenye urefu wa kilometa 13.07 kwa gharama ya Sh bilioni 16.32, pamoja na barabara ya Swaswa-Mpamaa hadi kuunganisha barabara kuu ya Arusha yenye urefu wa kilometa 8.20 kwa gharama ya Sh bilioni 9.5.

Nyingine ni uboreshaji barabara ya mzunguko ya Mlimwa yenye urefu wa kilometa 5.80 kwa gharama ya Sh bilioni 7.9, pia barabara ya Kizota-Zuzu yenye urefu wa kilometa 15.3 kwa gharama ya Sh bilioni 16.9.

Pia utahusisha barabara ya kijamii ya Chidachi yenye urefu wa kilometa 27.32 kwa gharama ya Sh bilioni 35.22 pamoja na barabara ya Ilazo yenye urefu wa kilometa 14.44 kwa gharama ya Sh bilioni 18.12 pamoja na barabara ya Nytuka hadi Chuo Kikuu cha Udom yenye urefu wa kilometa 3.11 kwa gharama ya Sh bilioni 3.5.

Pia fedha hizo zitatumika kujenga barabara ya Iyumbu yenye urefu wa kilometa 43 kwa kiwango cha lami kwa gharama ya Sh bilioni 89.6 na barabara ya Mtumba-Kikombo yenye urefu wa kilometa 108 kwa gharama ya Sh bilioni 223.42.

Ujenzi wa kiwango cha lami pia utahusisha barabara ya Nala yenye urefu wa kilometa 35.88 kwa gharama ya Sh bilioni 74.8, barabara ya Mahungu yenye urefu wa kilometa 15.21 kwa gharama ya Sh bilioni 28.01 na barabara ya Nzuguni yenye urefe wa kilometa 36.7 kwa gharama ya Sh bilioni 76.56.

Pia utahusisha ujenzi wa barabara ya Mkalama yenye urefu wa kilometa 29.9 kwa kiwango cha lami kwa gharama ya Sh bilioni 62.7 pamoja na barabara ya Mapinduzi yenye urefu wa kilometa 20.6 kwa gharama ya Sh bilioni 43.4.

 

BENKI ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imepongeza uthubutu ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi