loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

JPM kufungua mradi wa maji Ziwa Victoria wa bilioni 617/-

RAIS John Magufuli atafanya ziara ya siku moja mkoani Tabora na kufungua mradi mkubwa wa maji wa Ziwa Victoria ulioigharimu serikali Sh bilioni 617.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tabora jana, mkuu wa mkoa huo, Dk Philemon Sengati alisema Rais Magufuli anatarajiwa kufanya ziara hiyo keshokutwa.

Alisema fedha za mradi huo mkubwa wa maji kutoka Ziwa Victoria uliogharimu Sh bilioni 617 zilizotolewa na Benki ya EXIM ya India.

Alisema mradi huo wa maji utanufaisha wananchi milioni 1.1 katika wilaya za Nzega, Igunga, Uyui na Manispaa ya Tabora.

Dk Sengati akiwa mkoani humo, Rais Mgufuli pia ataweka alisema jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la magonjwa ya dharura katika Hospitali ya Rufaa Kitete ambao utagharimu Sh milioni 600 hadi kukamilika kwake.

Alisema katika kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Tabora, serikali ilitoa Sh bilioni 481.6 kwa ajili ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami na upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Tabora.

Mkuu huyo wa mkoa alisema Rais Magufuli pia atahutubia wananchi katika viwanja vya mpira wa miguu wa Ally Hassan Mwinyi na kuwataka wananchi wajitokeze kwa wingi ili wakamsikilize.

 

BENKI ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imepongeza uthubutu ...

foto
Mwandishi: Lucas Raphael, Tabora

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi