loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Serikali kutoa kauli utapeli mitandaoni, bando la simu

SERIKALI inatarajia kuja na kauli kuhusiana na utapeli wa mitandao na changamoto za vifurushi (bando) kwa wateja wa simu za mkononi nchini.

Hayo yalisemwa jijini Dodoma jana na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habri, Faustine Ndugulile wakati akifungua mkutano kati yake na watendaji wakuu wa kampuni za simu nchini.

“Kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wateja kuhusiana na utapeli wa kimtandao na changamoto za vifurushi. Tunaendelea na mazungumzo ya ndani na wakuu wa kampuni hizo kujadiliana kuhusiana na changamoto hizo.”

"Niwatoe wasiwasi Watanzania wote wanaouliza tumefikia wapi kuhusiana na masuala hayo, wasihofu muda si mrefu tutakuja na majibu na ufumbuzi wa kina," alisema.

Alisema kumekuwa na wimbi kubwa la wizi kwa njia ya mtandao lakini wizara hiyo inakwenda kumaliza tatizo hilo muda si mrefu.

Ndugulile alisema baada ya mazungumzo hayo kukamilisha, wizara itakuja na kauli ya serikali juu ya namna ilivyojipanga kutatua na kumaliza malalamiko hayo ya wateja kwa kutoka na maazimio ya kina.

"Maelekezo haya ya kuhakikisha Watanzania wote wanapata huduma ya mawasiliano na huduma za simu na huduma za mtandao yemeelezwa na kuainishwa kwenye Ilani ya CCM, hivi sisi kama wasaidizi wa Rais John Magufuli tunapaswa kuyatekeleza na kufikia malengo yaliyokusudiwa," alisema.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Justina Mashiba alisema wamewakutanisha wadau hao ambao ni watoa huduma za mawasiliano ili waweze kujadiliana na kuona namna wanavyoweza kufikia malengo yaliyokusudiwa katika kufikisha huduma hizo kwa Watanzania wote.

SERIKALI imeiruhusu sekta binafsi kuingiza nchini matrekta madogo ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi