loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Murray atabiriwa makubwa 2021

JAMIE Murray ana amini kuwa kaka yake, Andy anaweza kurejea kucheza katika kiwango cha juu na anafikiri mwaka huu utakuwa mkubwa kwake.

Murray mwenye umri wa miaka 33 ambaye ni bingwa mara tatu wa mashindano makubwa ya tenisi duniani, alilazimika kujitoa katika mashindano ya mwezi ujao ya Australian Open baada ya kukutwa na covid-19.

"Amefanya vizuri kufikia hatua hii kwani atarejea pale atakapohisi kuwa katika nafasi nzuri ya kushindana na wachezaji bora duniani.”

"Ni wazi itakuwa imemchanganya kwa sababu alikuwa na kipindi kibaya kwa muda mrefu,” alisema.

Mwaka huu mashindano ya Australian Open ni ya tatu katika kipindi cha miaka minne Murray kutoshiriki mara ya tisa kati ya mashindano 13.

Alilosa michezo saba rasmi mwaka jana kwa sababu mbalimbali, ikiwamo mlipuko wa virusi vya corona uliosababisha tenisi pamoja na michezo mingine kusimama.

"Hata mwaka 2020 wakati aliporejea katika ubora wake alikuwa tayari kurudi kushindana huko Miami, lakini covid-19 iliibuka na mashindano hayo yalifutwa na  kuwa na miezi mingine mitano au sita ya mapumziko.” alisema Jamie.

"Hivyo ilikuwa ngumu kwake lakini nafikiri sasa yuko katika nafasi nzuri. Ni wazi mwaka huu ni mzuri kwake ikiwa ataendelea kuwa fiti, mwenye afya na kama atacheza mashindano yote yaliyopo katika kalenda ya mwaka,” alisema Jamie.

KOCHA wa Tottenham Spurs, Jose Mourinho amesema kwamba kila kitu ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi