loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tuchel achukua mikoba ya Lampard

KLABU ya Chelsea imemtangaza kocha wa zamani wa Paris St-Germain (PSG) ya Ufaransa, Thomas Tuchel kuwa kocha wake mpya akichukua nafasi ya Frank Lampard aliyetupiwa virago.

Kocha huyo alishinda mataji mawili ya ligi, Kombe la Ligi na Kombe la Ufaransa wakati akiifundisha PSG.

''Siwezi kusubiri kukutana na timu yangu mpya na kuanza ushindani katika ligi yenye ushindani mkubwa katika soka. Nashukuru kuwa mmoja wa wanafamilia wa Chelsea,'' alisema Tuchel mwenye umri wa miaka 47.

Chelsea ilimtupia virago Lampard Jumatatu iliyopita baada ya kipindi kigumu cha miezi 18, akishinda mechi moja kati ya tano za Ligi Kuu msimu huu.

"Sote tunaheshimu kazi ya Lampard na heshima aliyoiacha Chelsea," alisema Tuchel.

Raia huyo wa Ujerumani sasa atakuwa kocha wa 11 kuajiriwa na mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich tangu bilionea huyo alipoinunua klabu hiyo.

Mkurugenzi wa Chelsea, Marina Granovskaia amemtaja Tuchel kama mmoja wa makocha bora zaidi Ulaya, huku akisema wana mambo mengi ya kufanya msimu huu na baadae.

Kocha huyo mpya jana alitarajiwa kuwa katika benchi la Chelsea wakati ilipocheza na Wolves katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.

Akiwa Chelsea, jukumu kubwa la kocha huyo litakuwa ni  kuhakikisha timu hiyo inamaliza ndani ya nne bora ili iweze kufuzu moja kwa moja katika Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya wiki iliyopita kupata kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Leicester City.

 

Nguli wa Manchester United, Paul Scholes amemshauri kiungo ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi