loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

City yaisambaratisha 5-0 West Bromwich  

MANCHESTER City imeshika uongozi wa msimamo wa Ligi Kuu ya England baada ya kuisambaratisha West Bromwich Albion kwa mabao 5-0.

Washindi wa mchezo huo walikuwa ugenini na hadi kipindi cha kwanza kinamalizika walikuwa mbele kwa mabao 4-0 kabla ya kufunga la tano katika kipindi cha pili kwa bao la dakika 57.

Katika historia ya ligi kubwa Ulaya, hakuna timu yoyote iliyowahi kuruhusu kufungwa mabao mengi nyumbani kama Albion inayofundishwa na kocha, Sam Allardyce.

Kichapo hicho kinaifanya West Brow kuwa katika nafasi ya 19 ikiwa na pointi sita kutoka katika ukanda salama wakati ikielekea kucheza mchezo wake wa Jumamosi dhidi ya Fulham.

Man City ilicheza bila ya baadhi ya wachezaji wake tegemeo kama Kevin de Bruyne, Sergio Aguero na Gabriel Jesus.

Kocha wa Man City, Pep Guardiola alimuelezea  Allardyce kama mtu mwenye akili nyingi kabla ya mchezo huo.

Ni kama wiki sita zimepita tangu Albion ilipoibana Man City na kutoka nayo sare huko Manchester katika usiku ambao kipa Sam Johnstone alicheza vizuri.

 

KOCHA wa Tottenham Spurs, Jose Mourinho amesema kwamba kila kitu ...

foto
Mwandishi: MANCHESTER, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi