loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Putin, Biden wafufua mkataba alioukataa Trump

RAIS Vladimir Putin wa Urusi na mwenzake wa Marekani, Joe Biden wameeleza kuridhika kutokana na kufufuliwa kwa Mkataba Mpya wa START.

Kwa mujibu wa mtandao wa habari wa Ikulu ya Urusi, marais hao walifanya mazungumzo yao kwa simu wiki hii.

“Marais walionesha kuridhika katika majadiliano yao ya  kidiplomasia juu ya makubaliano ya kuongeza Mkataba Mpya wa START. Pande zote zinakamilisha ndani ya siku chache, zitakamilisha taratibu zinahitajika kuhakikisha utendaji zaidi wa utaratibu huu wa kimataifa wa upeo wa kurudisha silaha za nyuklia,” ilisema taarifa hiyo.

Mkataba kati ya Marekani na Shirikisho la Urusi kuhusu hatua za Kupunguza Silaha za Mkakati (Mkataba Mpya wa START) ulisainiwa mwaka 2010 na kuanza kutumika Februari 5, 2011.

“Kwa ujumla, mazungumzo kati ya viongozi wa Urusi na Marekani yalikuwa ya biashara na ya asili ya kweli,” iliongeza taarifa hiyo.

Viongozi hao wawili walionekana kutia saini makubaliano ya kurejesha mkataba wa New Start, yaliyofanyika wakati wa utawala wa Rais Barack Obama ambayo yanapunguza viwango vya silaha, makombora na virusha makombora miongoni mwa silaha za nyuklia za Marekani na Urusi.

Mkataba huo ulipaswa kumalizika mwezi ujao, na aliyekuwa Rais wa Marekani, Donald Trump alikataa kusaini.

foto
Mwandishi: MOSCOW, Urusi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi