loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

DCEA kuzindua kituo cha tiba Arusha

MAMLAKA   ya Kudhibiti  na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), inatarajia kuzindua kituo cha tiba ya methodone mkoani Arusha Februari 15,2021.

Kamishna Jenerali wa DCEA, James Kaji amesema kituo hicho cha Methodone kitahudumia Kanda za Kaskazini.

Amesema pia wameongeza wigo wa upatikanaji wa tiba ya uraibu wa dawa za kulevya kwa kuongeza vituo vingine vitatu vya kutolea tiba ya methadone jijini Dar es Salaam.

Ametaja vituo hivyo ni Segerea, Mbagala rangi tatu na Tegeta ambayo vinatarajiwa kuanza kutoa huduma kuanzia  mwezi ujao  Februari mwaka huu.

Amesema kuanzishwa kwa vituo hivyo kutafanya Mkoa wa Dar es Salaam kuwa na vituo sita vinavyotoa tiba ya methoone ili kupunguza msongamano uliokuwa katika vituo vya awali.

Kaji amesema Mikoa mingine iliyokuwa na vituo vya tiba ya methodone ni Mbeya, Mwanza na Dodoma  na kwamba hadi sasa vituo hivyo vimeweza kutoa huduma kwa waraibu 9,500.

Amesema mbali na vituo pia huduma ya upataji nafuu katika nyumba 25 ‘sober houses’ zilizopo maeno mbali mbali  nchini hadi kufikia mwezi Desemba 2020, kulikuwa na waraibu 3,663 walionufaika na huduma hiyo kati yao wanawake ni 74, na wanaume ni 3,609.

SERIKALI imeiruhusu sekta binafsi kuingiza nchini matrekta madogo ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi