loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

JPM: Wabunge, wabaneni Mawaziri ili wafanye kazi

RAIS John Pombe Magufuli amewataka wabunge wawabane mawaziri kwa kuwahoji ili wawajibike kutatua kero za wananchi.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo alipokuwa akizindua Kituo cha afya cha Mbogwe,  mkoani Geita.

Amesema, “Nataka mawaziri wangu wahojiwe...wajue wajibu wao, kazi ya mbunge ni kuhoji na hata kukataa bajeti ili kuleta uwajibikaji ndani ya serikali, mimi nataka wawabane ili matatizo ya wananchi yatatuliwe."

Kauli hiyo imekuja baada ya Mbunge Nicodemus Maganga – Jimbo la Mbogwe Geita kudai kuna ulipuaji kwenye baadhi ya miradi.

"Nakubaliana na mbunge (Nicodemus Maganga – Jimbo la Mbogwe Geita) kuwa hata rangi imepakwa usiku usiku, nimeona kuna mahali hata sementu bado imemwagika chini ingekuwa ni ya zamani  niliyoyaona yasingeonekana, ila nimeridhika na majengo," alisema Rais Magufuli

“Nilipofika hapa (kwenye uzinduzi), Waziri wa Tamisemi Jafo (Seleman)  na Waziri wa Afya Gwajima (Doroth), na Mkurugenzi wamenipeleka kwenye jengo nilitaka nijiridhishe thamani ya milioni 400 zilipotumika, kwa maelezo niliyopewa nimeridhika, ingawa kuna mambo nimeyaona nimeamua tu kunyamaza.”

Katika hatua nyingine amewataka viongozi kuacha nidhamu ya uoga na badala yake wanapaswa kutekeleza yale ambayo wanaweza kuyafanya na kwamba hapendi kudanganywa.

“Niwaombe watendaji wangu msiwe na nidhamu ya uoga, tekeleze yale yanayowezekana, yasiyowezekana msiharibu zaidi sipendi kudanganywa kwa sababu uwa naumia sana, lakini niwapongeze majengo yamekamilika,” alisema na kuongeza

SERIKALI imeiruhusu sekta binafsi kuingiza nchini matrekta madogo ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi