loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Nizar aahidi makubwa Yanga

KOCHA Msaidizi mpya wa Yanga, Nizar Khalifan amesema amejiunga na timu hiyo kushirikiana na benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze kuhakikisha miamba hiyo inachukua taji la Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mchezaji huyo wa zamani wa Yanga alitambulishwa rasmi Dar es Salaam jana pamoja na kocha mpya wa viungo, Edem Mortotsi raia wa Ghana anayetokea Canada.

Akizungumza baada ya kutambulishwa, Nizar alisema atasaidiana kwa nguvu na akili yake yote na viongozi waliopo kutoa alichonacho kuendeleza dhamira ya klabu hiyo.

“Nimshukuru Mungu kwa kupata nafasi hii, tulikuwa watano tulioomba lakini nimebahatika mimi, tutasaidiana kwa hali na mali kuendeleza dhamira ya Yanga,” alisema.

Nizar aliyekuwa kocha wa timu ya daraja la kwanza ya African Lyon amewahi kuzichezea timu mbalimbali kama Singida United, Pamba, Moro United na Vancouver Whitecaps ya Canada.

Anachukua nafasi ya Juma Mwambusi aliyeomba kupumzika kutokana na matatizo ya kiafya. Wakati huo huo, klabu hiyo jana ilimtambulisha Mortotsi kuwa kocha wa viungo.

Mortotsi aliwahi kuichezea klabu ya FC Edmonton ya Canada kwa miaka saba. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 27 alikuwa kiungo wa kati aliyewahi kucheza mechi 18 za mashindano yote msimu wa 2018/2019. Msimu uliopita hakufanikiwa kucheza kutokana na kusumbuliwa na majeraha.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi