loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

DCEA yashinda Kesi tatu za Mapapa wa Dawa za Kulevya

MAMLAKA   ya Kudhibiti  na Kupambana na Dawa za Kulevya  nchini, imesema katika kipindi cha Mwezi Novemba na Desemba 2020, imefafanikiwa kushinda kesi tatu kubwa  za   wafanyabiashara maarufu wa  dawa za kulevya nchini.

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti  Dawa za Kulevya (DCEA), James Kaji,  amesema kesi hizo zilikuwa zikisikilizwa katika Mahakama  ya Uhujumu Uchumi,  ambapo DCEA ilishinda baada ya mahakama hiyo kumtia hatiani Yanga Omari Yanga maarufu ‘Rais wa Tanga’  na kumuhukumu  kifungo cha miaka 30 baada ya kukutwa na hatia ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroine uzito wa gramu 1052.63

Yanga alikamatwa  Agosti, 2018 na wenzake  wawili mtaa  wa Bombo jijini Tanga, wakitaka kusafirisha dawa hizo za kulevya.

Pia mfanyabiashara mwingine aliyetiwa hatiani ni Ayubu Mfaume maarufu ‘Kiboko’ na mkewe Pili Kiboko  ambao wamehukumiwa miaka 20 jela kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin zenye uzito wa gramu 251.25.

Kiboko  anadaiwa kuwa  kiongozi wa ulanguzi wa dawa ya kulevya aina ya heroine amekuwa akifanya operesheni zake kati ya Afrika mashariki na China.

“Kiboko ana vijana 68 ambao wameshikiliwa China, ameharibu maisha ya vijana wengi,” amesema Kaji na kueleza kuwa amekuwa na ushirikiano na walanguzi wa mihadarati nchini Brazil, Pakistani, na Mataifa ya Ulaya.

Pia raia wawili wa Iran nao wametiwa hatiani kwa kosa  la kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin yenye uzito  wa gramu 111.02 katika Bahari ya Hindi na kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela pamoja na kutaifishwa kwa jahazi husika.

 

SERIKALI imeiruhusu sekta binafsi kuingiza nchini matrekta madogo ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi