loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Moi yaanza Uchunguzi wa Ubongo bila kufungua fuvu la kichwa

TAASISI ya Mifupa Muhimbili(MOI) kwa mara ya kwanza imeanza kutoa huduma ya uchunguzi wa mishipa ya damu kwenye ubongo bila kufungua fuvu la kichwa.

Uchunguzi huo umefanywa kwa saa tatu katika maabara ya kisasa  ya upasuaji wa ubongo na jopo la madaktari bingwa, wauguzi, watalamu wa radiolojia wazalendo sita kutoka MOI, Hospitali ya Taifa Muhimbili(MNH) na Taasisi ya Moyo ya jakaya Kikwete(JKCI) pamoja na Hospitali ya Agakhan.

Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dk Respicious Boniface amesema kuanza kwa maabara hiyo ni ishara ya mageuzi makubwa katika sekta ya afya hapa nchini kwani maabara kama hiyo haipo  kwenye nchi nyingine kwenye ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

“Leo ni siku ya furaha sana kwani tumeanza kutumia maabara yetu ya upasuaji wa ubongo, hii imewezekana kutokana na dhamira ya dhati ya Rais John Magufuli ya kuboresha huduma za afya hapa nchini kwani maabara hii imejengwa Serikali ya awamu ya Tano kwa zaidi ya Sh bilioni 7.9,”alisema Dk Boniface

SERIKALI imeiruhusu sekta binafsi kuingiza nchini matrekta madogo ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi