loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Walimu wanaofundisha ‘tuisheni’ kukiona

WALIMU Wakuu wa shule za msingi wameagizwa kusimamia vizuri taaluma na kuwabaini wale wote wanaojikita kufundisha tuisheni badala ya kutumikia ajira waliyoiomba.


Hayo yamebainishwa leo na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako ambapo alitoa agizo wakati alipokuwa akifungua mafunzo ya Utibiti Ubora wa Shule wa Ndani kwa Wakuu wa Shule za Msingi yaliyofanyika Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM), Bagamoyo.


Ndalichako alisema walimu wanaojikita kwenye tuisheni wamekuwa wakitaja shule wanazofundisha kama anuani yao ya kufanya waaminike kwa wazazi ama walezi huku wakiwa hawatumikii eneo lao la ajira kwa uaminifu.


"Upo mtindo wa baadhi ya walimu kujikita kwenye tuisheni, shuleni wanakofundisha ni kama dawati awe na anuani ya kutambulika yeye ni mwalimu wa shule Fulani lakini mawazo yake yote yapo katka kufanya tuisheni.


"Naomba sana walimu wangu wakuu muweze kusimamia vizuri taaluma na kuangalia nidhamu ya walimu wenu katika kufanya kazi ambayo wanatakiwa kuifanya," amesema Waziri huyo.


Aidha aliwataka walimu wakuu kusimamia utekelezaji wa mtaala, kusimamia rasilimali za shule, kuandaa na kusimamia utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya shule na kuhakikisha kuna mazingira rafiki ya kufundishia na kujifunzia.


Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa ADEM, Dk. Siston Masanja alisema mafunzo hayo ya uthibiti ubora wa shule kwa walimu wakuu wa shule za msingi yanafanyika nchi nzima kwa awamu mbili yakihusisha walimu wakuu 16,223.


Alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wa kusimamia ubora wa shule na kutekeleza majukumu ya uthibiti ubora wa shule wa ndani kwa kuzingatia viwango vya elimu vilivyobainishwa katika kiunzi cha uthibiti ubora wa shule.

NAIBU Waziri wa Mawasiliano na ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi, Bagamoyo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi