loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Simba kupaki basi Congo

KOCHA wa Simba, Didier Gomes amewaambia wachezaji wake kukaba zaidi katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DR) utakaofanyika kesho nchini humo.

Simba itaingia kwenye mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kichapo kikali cha mabao 5-0  msimu wa mwaka juzi kwenye hatua kama hiyo.

Akizungumza Dar es Salaam juzi, Gomes alisema wanaenda kucheza mchezo huo wa ugenini wakiwa na malengo.

“Tunafahamu fika tunapaswa kufanya marekebisho tunapokosea.”

“Mchezo uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Azam wachezaji wangu walicheza kwa kuwapa nafasi wapinzani wetu na kupata mabao, nimewapa maelekezo kwenye mazoezi ili kuzidisha nidhamu michezo yote ya ugenini katika kujilinda.”

“Na mfahamu kocha wa AS Vital na vilevile nilichukua muda kufutilia video ya michezo ya As Vital na Al Ahly  tunahitaji kuja na mfumo mpya wa kuzidisha nidhamu mechi za ugenini kuanza kutengeneza rekodi mpya kwani tunapoteza kwa mabao mengi ,”alisema Gomes.

“Kwenye mchezo huo tunahitaji kushinda lakini hatuwezi kusahau majukumu ya kujilinda kwa wachezaji wote kusaidiana majukumu kwa muda wote kwakuwa wapinzani wetu watahitaji kushinda kwao,” alisema.

Gomes alisema beki wake mpya, Peter Muduhwa yupo tayari kwa mchezo huo pamoja na Joash Onyango aliyepata majeraha kwenye mchezo uliopita wa ligi na kwamba wachezaji wote wana afya njema.

Simba imepangwa Kundi A kwenye michuano hiyo pamoja na As Vita, Al Ahly ya Misri na Al Merrikh ya Sudan.

TIMU ya Soka ya Dodoma Jiji ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi