loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wazushi, matapeli mitandaoni kukiona

WIZARA ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imetangaza kuwa kuanzia leo itaanza kuwashughulikia wapotoshaji kwenye mitandao wakiwemo wanaorudia kutuma taarifa za uongo zilizotumwa na watu wengine.

Waziri wa wizara hiyo, Dk Faustine Ndugulile, alisema Dar es Salaam kuwa, watakaoshughulikiwa ni matapeli kwenye mitandao, wanaotoa taarifa za uzushi, uchochezi, na uzandiki.

“Nadhani Mheshimiwa Rais mmemsikia, na sisi tumeshakubaliana kuanzia Jumatatu tutaanza kuchezesha watu muziki. Kwa hiyo nitoe rai kwa Watanzania kama huna uhakika na kile unachokisema usiposti, usiritwiti, usilaiki, usifanye chochote na wala usikomenti”alisema Dk Ndugulile.

Alisema wamedhamiria kuwashughulikia watu hao na kwa kuwa wizara hiyo ni mpya wanaendelea kuboresha mifumo ya ndani.

‘Tutatoa namba mahususi za watu kulalamika kuhusiana na utapeli unaoendelea katika mtandao hiyo taarifa tutaitoa lakini tunataka vilevile tutoe taarifa na tutaanzisha zoezi la uhakiki wa namba zote za simu tena upya ili sasa tuweze kubaini wale wote wanaoendelea kufanya hizi shughuli za utapeli na kuchukua hatua”alisema Dk Ndugulile.

Wakati huohuo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa jana alionya wanaotumia mitandao ya kijamii kutoa lugha za matusi, kuudhi na pia kusambaza za uongo na upotoshaji.

Alisema jijini Arusha kuwa kufanya hivyo ni kinyume na kanuni za maudhui mtandaoni za 2018 zinazozuia watumiaji wa mitandao kufanya vitendo hivyo.

Bashungwa alitoa onyo wakati wa kongamano la fursa kwa wanamuziki lililoandaliwa na taasisi ya kijamii inayoshughulika na wanamuziki (TAMUFO).

Julai 17 mwaka jana serikali ilichapisha mabadiliko ya Kanuni za Maudhui Mtandaoni kwenye gazeti la Serikali kupitia gazeti Na. 29 Toleo la 101.

Mabadiliko hayo kupitia notisi Na. 538 yanabadilisha baadhi ya kanuni za maudhui mtandaoni za mwaka 2018 kuhakikisha zinalinda maslahi ya watumiaji wa mitandao.

Kuhusu vifurushi kwenye simu za mkononi Dk Ndugulile alisema, Februari 28 mwaka huu serikali itatoa tamko kuhusu jambo hilo. Alisema suala hilo linahitaji umakini hivyo wananchi wavumilie hadi siku hiyo serikali ita- kapotoa suluhisho la kudumu kuhusu jambo hilo.

“Kuna kazi inaendelea kuchakatwa na hata leo nitakuwa napata taarifa ya mwendelezo wa jambo hili kwa hiyo Watanzania waendelee kutuvumilia wawe na subira ifikapo tarehe 28 mwezi huu tutakuja na taarifa kamili ya nini tunakwenda kufanya kuhusiana na vifurushi” alisema Dk Ndugulile.

Mwanzoni mwa mwezi huu, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), James Kilaba, alitoa waraka wa mashauriano kuhusu kuandaa kanuni ndogo za vifurushi, ofa na promosheni kwenye huduma za mawasiliano ya simu.

Katika waraka huo TCRA ilikaribisha kutoka kwa watumiaji na wadau kuhusu mfumo mwafaka wa kusimamia uwekaji wa vifurushi vya huduma za mawasiliano ya simu na gharama za tozo za vifurushi.

Uongozi wa TCRA ulieleza kuwa watumiaji wa huduma za mawasiliano wamekuwa wakilalamika kuhusu namna vifurushi vya huduma hizo vinavyopangwa na kutolewa.

“TCRA ingependa kupata maoni yako na hoja kuanzia sasa hadi saa kumi 10 jioni tarehe 17 Februari 2021…”ilieleza taarifa ya Kilaba.

Ilitaja miongoni mwa malalamiko hayo kuwa ni kukosekana uwazi katika makato ya data wakati wa kutumia vifurushi, kuisha kwa kasi kwa vifurushi vya data, na matangazo ya huduma yanayopotosha na vigezo na masharti visivyo bayana.

TCRA ilitaja mambo mengine kuwa ni kuunganishwa moja kwa moja kifurushi baada ya kifurushi alicholipia mteja kufikia ukomo wa muda wa matumizi au kinapoisha, kuunganisha watumiaji kwenye vifurushi bila ridhaa yao, na watumiaji kupoteza muda wa maongezi, idadi ya meseji (SMS) au data ambazo hawajazitumia baada ya ukomo wa muda wa kifurushi.

NAIBU Waziri wa Mawasiliano na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi