loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Walimu 159 wastaafu kwa hiyari Julai- Desemba

WALIMU 988 wamestaafu kati ya Julai hadi Desemba mwaka jana wakiwemo 817 waliostaafu kwa lazima, 159 kwa hiyari, na 12 kwa sababu ya ugonjwa.

Akizungumza na HabariLeo jijini Dodoma, Kaimu Katibu Mkuu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Moses Chitama, alisema, kati ya walimu hao, 872 ni wa shule za msingi, na 116 wa shule za sekondari.

Chitama alisema walimu 727 walistaafu kwa lazima katika shule za msingi wakiwemo wanaume 354 sawa na asilimia 48.7 na wanawake ni 373 sawa na asilimia 51.3.

Alisema walimu 135 wa sekondari walistaafu kwa hiyari wakiwemo wanaume 72 sawa na asilimia 53.3 na wanawake 63 sawa na asilimia 46.7.

Chitama alisema, walimu 10 wa shule ya msingi walistaafu kwa ugonjwa wakiwemo  wanaume saba sawa na asilimia 70, na wanawake watatu sawa na asilimia 30.

Alisema walimu 90 wa shule za sekondari walistaafu kwa lazima wakiwemo wanaume 43 sawa na asilimia 47.8 na wanawake 47 sawa na asilimia 52.2.

Chitama alisema, walimu 24 wa sekondari walistaafu kwa hiyari wakiwemo wanaume 15 sawa na asilimia 62.5 na wanawake tisa sawa na asilimia 37.5.

Alisema, katika miezi hiyo sita walimu wawili wa sekondari wanawake walistaafu kwa ugonjwa.

Chitama alisema, walimu wanaume 491 walistaafu kati ya Julai hadi Desemba mwaka jana wakiwemo 397 waliostaafu kwa lazima, 87 kwa hiari, na saba kwa ugonjwa.

"Jumla ya wanawake waliostaafu katika kipindi hicho ni 497, kati yao 420 sawa na asilimia 84.5 waliostaafu kwa lazima, 72  sawa na asilimia 14.5 kwa hiari na watano sawa na asilimia 1.0 kwa ugonjwa," alisema.

Kwa kuzingatia takwimu hizo walimu wanaume waliostaafu kwa lazima, hiyari na ugonjwa ni 491 na wanawake 497 walistaafu kwa sababu hizo.

BENKI ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imepongeza uthubutu ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi