loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kalemani: Huu si muda wa kujadiliana JNHPP

WAZIRI wa Nishati, Dk Medard Kalemani, amewataka wakandarasi wanaojenga mradi wa kufua umeme kwenye bwawa la Julius Nyerere (JNHPP), Arab Contractors na Elsewedy Electric kutoka Misri watekeleze maelekezo ya serikali yaliyomo katika mikataba ya uwekezaji kuhusu kuihudumia jamii (CSR).

Dk Kalemani, alitoa agizo hilo mwishoni mwa wiki, alipoumbelea mradi huo wilayani Rufiji, katika mkoa wa Pwani kukagua shughuli zinazoendelea hapo.

"Wakandarasi na wasimamizi wetu huu muda si wa kujadiliana , wataalamu sijadiliane na mkandarasi muda wa majadiliano ulishapita ndiyo maana mkataba ulisainiwa , sasa hivi ni unachapa kazi  ni utekelezaji wa kazi si muda wa majadiliano" alisema Dk Kalemani.

Alitaja baadhi ya kazi hizo kwa ni kujenga shule, kituo cha Afya, uwanja na ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilometa 41 kutoka Stesheni ya Tazara ya Fuga hadi kwenye mradi huo ianze kujengwa mara moja.

Waziri Kalemani, alisema anataka kuona maelekezo ya serikali katika CSR yanaanza kutekelezwa na hakuna muda wa majadiliano.

"Niwaombe sana wakandarasi, mhandisi na wataalamu msipoteze muda kujadiliana huku site hiyo nafasi ya kujadiliana haipo, nafasi iliyopo ni ya kuchapa kazi, kumsumbua mkandarasi ajue wajibu wake na tumalize kazi ndani ya muda , majadiliano yafikie mwisho" alisema.

Dk Kalemani pia alimtaka mkandarasi wa mradi huo upeleke wataalamu mahususi 13 waliobaki ili kufikia idadi ya 27 wanaopaswa kuwepo kulingana na mkataba.

"Nilipofanya ziara yangu hapa Desemba mwaka 2020, niliwakuta wataalamu mahususi wanne pekee na nikaagiza waliobakia 23 wanapaswa kufika haraka nchini ili kuungana na wenzao, nimeambiwa na mkandarasi ametekeleza kwa kuongeza 11 na kufikia 14" alisema na kuongeza;

"Nataka kuwaona wote 27 hapa kwenye mradi wale 13 nataka kuwaona, nimeambiwa na mkandarasi kuwa wengine wanafanyia kazi nje nje wapi nataka niwaone wote narudia tena ndani ya mwezi mmoja mhandisi wamefika kwenye mradi"

Dk Kalemani aliwashauri wakuu wa mikoa na wilaya wanaoguswa moja kwa moja na upatikanaji wa maji Mto Rufiji kuwa huu ni wakati wa kuongeza juhudi kuhamasisha wananchi walinde na kutunza vyanzo vya maji.

NAIBU Waziri wa Mawasiliano na ...

foto
Mwandishi: John Nditi, Rufiji

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi