loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Zaidi ya watoto 272 wa mtaani warejeshwa majumbani

ZAIDI ya watoto 272 waliokuwa wanaishi mitaani wamerejeshwa majumbani kwao. Hayo yalisemwa na Meneja mradi wa Shirika la Railway Children in Africa, Abdallah Issa.

Issa alisema kupitia mradi wa Kivuko ulioanza April 2018 na unatarajia kukamilika Machi 2021 wamefanikiwa kurejesha nyumbani watoto wa mitaani 272.

‘’Tutaendelea na mpango wa kurudisha majumbani watoto wa mitaani pamoja na kuwapatia mafunzo ya kujitambua pamoja na kuwapa miradi ya biashara’’ alisema Issa.

Issa alisema kupitia mradi huo wamepanga ndani ya mwaka huu mpaka mwezi Desemba watawarejesha majumbani watoto 200. Alisema kupitia mradi huo wameweza kuwasomesha watoto mashuleni pamoja na kuwapa vifaa vya shule ikiwemo madafatari.

Alisema kupitia mradi huo wameweza kutoa elimu ya ujasiriamali kwa vijana 221 ambapo kwa sasa vijana wengi wameweza kujiajari na kujipatia kipato chao katika kuendesha maisha yao.

Alisema wamefanikiwa pia kutoa huduma ya afya kwa watoto wa mtaani 537 mkoani Mwanza.

Mratibu kutoka Shirika la Cheka Sana,Domina Mabebe alisema shirika lao linashirikiana na Railway Children katika kuhakikisha wanarejesha watoto wa mtaani kwao pamoja na kuwapa Elimu.

Mlezi wa watoto kutoka Cheka Sana,Catherine Mikael kutoka Pasiansi alisema wamekuwa wakiwapowekea watoto wa mtaani na kukaa nao kisha kuwarejesha kwao.

Alisema watoto wengi wamekuwa na huzuni baada ya kutoka katika vituo vya malezi. Amewaomba wazazi kuhakikisha wanaacha tabia za ugomvi. Alisema ugumu wa maisha umepelekea kuwepo kwa watoto wa mitaani katika sehemu nyingi.

NAIBU Waziri wa Mawasiliano na ...

foto
Mwandishi: Na Alexander Sanga,Mwanza

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi