loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Barcelona waliniambia nimezeeka- Suarez

LUIS Suarez amesema jambo lililomkatisha tamaa zaidi na kuamua kuondoka Barcelona ni klabu hiyo kumwambia kwamba amekuwa mzee hawezi kucheza kwa kiwango cha juu. 

Suarez aliondoka Barca na kujiunga Atletico Septemba mwaka jana katika uhamisho ambao nyota wa Camp Nou Lionel Messi aliuelezea kama uliwavuruga.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 raia wa Uruguay yupo na furaha kwenye klabu yake ya sasa licha ya kusema kwamba huwa inamuwia vigumu kuwa mbali na familia yake. 

 “Kilichonikera zaidi ni waliponiambia nilikuwa mzee hivyo siwezi tena kucheza kwa kiwango cha juu.” 

“Hilo sikulipenda kabisa. Kama ningekuwa sijafanya chochote katika klabu kama Barca kwa misimu mitatu au minne, ningeelewa.”  

“Lakini kila mwaka Barca nilifunga mabao zaidi ya 20 kwa msimu. Mara zote nimekuwa na takwimu nzuri, nyuma ya Leo (Messi).” 

“Leo tunaona kwamba sio rahisi kucheza Barca, wachezaji wengi waliosajiliwa pale hawana kiwango walichokitarajia, mimi nimecheza kwa miaka sita Barca nikilinda kiwango changu na kufanya kile walichokitarajia nikifanye,” alisema.

Suarez yuko sahihi kwamba kila msimu Barcelona alifunga mabao zaidi ya 20.

Msimu wa mwaka 2015/16 alifunga mabao 59 kwenye michuano yote.

Ni msimu aliofunga mabao mengi zaidi ya Messi na kushinda kiatu cha dhahabu Ulaya. 

Msimu wa mwaka 2016/17 alifunga mabao 36 na msimu wa mwaka 2017/18 alifunga mabao 31 na misimu yake miwili ya mwisho alifunga mabao 23 na 21.

KOCHA Atalanta Gian Piero Gasperini amesema mwamuzi aliharibu ...

foto
Mwandishi: MADRID, Hispania

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi