loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Samia ataka mikakati misitu, nyuki vikuze uchumi

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan ameagiza wanasayansi na wataalamu wa misitu na nyuki kuchambua changamoto zinazoikabili sekta hiyo ili ichangie kwenye mapinduzi ya kiuchumi kupitia viwanda.

Samia alitoa maagizo hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akifungua Kongamano la Kimataifa la Sayansi kuhusu mnyororo wa thamani wa mazao ya misitu na nyuki kwa maisha endelevu na uchumi wa viwanda. 

Makamu wa Rais aliwakilishwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Damas Ndumbaro.

Samia aliagiza wataalamu waangalie suala la kuwa na viwanda vingi zaidi vinavyotumia malighafi za ndani za misitu na nyuki na pia kuangalia umuhimu wa sekta ya misitu na nyuki kuongeza mchango wake katika mapato ya nchi. 

Hivi sasa sekta hiyo inachsngia asilimia 3.5 katika Pato la Taifa (GDP) na asilimia 5.9 kwa mapato yote yanayotokana na biashara ya nje.

Samia, aliagiza kongamano hilo lije na mkakati wa kunadi bidhaa za misitu na nyuki kwa kuangalia maeneo makuu matatu ikiwamo kuweka mkakati wa kuboresha uzalishaji kwa idadi na viwango ili bidhaa ziwe na ubora wa hali ya juu, kutambua na kutafuta ufumbuzi wa changamoto zilizopo katika mnyororo wa thamani ya mazao ya misitu na nyuki na kuanisha masoko.

“Tanzania ina wasomi wengi sana na tafiti nyingi sana za mazao ya misitu na nyuki zilizofanywa na Tafori (Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania) na Tawiri, lakini nyingi zimewekwa makabatini. Tafiti hizi zinapaswa kufika kwa wadau walio katika jamii tena ziandikwe kwa lugha nyepesi wanayoielewa,” aliagiza Samia.

Alitaka pia changamoto za uvamizi wa misitu unaotokana na kilimo, mbao, mkaa, nguzo na mabadiliko ya tabianchi ziangaliwe na kutoa majibu yake.

Alisema bado rasilimali za misitu na nyuki hazijatumiwa vizuri na kutoa mfano kuwa uwezo wa kuzalisha asali ulionao Tanzania ni tani 134, lakini hivi sasa inazalishwa tani 34 pekee huku tani 100 hazizalishwi.

Aliagiza eneo hilo lichambuliwe na wataalamu hao kupitia  Ibara ya 46, 67-71, 234- 235 za Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya 2020-2025 hasa Ibara ya 46 inayozungumzia mnyororo wa thamani wa mazao ya misitu.

Samia aliagiza washiriki wa kongamano hilo kuchambua hotuba ya Rais John Magufuli alipozindua Bunge, Novemba 13, mwaka jana ambayo pamoja na mambo mengine imeelekeza kupitia Ilani kila halmashauri ipande miti milioni 1.5 kwa mwaka.

Maagizo mengine ni kuongeza viwanda vya mazao ya nyuki vifike angalau 200 vidogo ambapo hivi karibuni vipo 21. 

Hata hivyo, viwanda vitano vinatarajiwa kuongezeka hivi karibuni. 

Pia kuongeza viwanda vya mazao ya misitu zaidi ya 4,200 vilivyopo sasa na tija katika uzalishaji na ubora wa bidhaa zake.

Samia alipongeza wadau wa misitu kwani viwanda hivyo vimepunguza uagizaji wa  bidhaa nje ya nchi ambapo mwaka 2015 bidhaa za mbao za mita za ujazo 95,000 ziliagizwa kutoka nje wakati mwaka 2020 ziliagizwa za mita za ujazo 25,000 ikiwa ni punguzo za mita za ujazo 70,000. 

Zilizosafirishwa nje pia zimeongezeka kutoka mita za ujazo 33,000 mwaka 2015 hadi 90,000 mwaka 2020.

Aliagiza wadau wasimamie kuhifadhi na utunzaji mazingira kupitia Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 huku akisisitiza kuwa sekta ya mazingira iliyo chini ya ofisi yake ni muhimu kwa uchumi wa nchi kwa kuwa vyanzo vya umeme ni maji ambayo yanategemea utunzaji mazingira.

Samia aliagiza watu waache kuchunga mifugo na kulima katika hifadhi za misitu na kulitaka Jeshi Usu la Hifadhi ya Misitu na Wanyamapori alilolizindua Novemba 17, 2018, lifanye kazi yake.

Aliwashukuru wadau wa maendeleo ikiwamo Finland kwa kushiriki katika kukuza sekta ya misitu na nyuki na aliagiza mipango miwili ya kitaifa ya Utafiti wa Misitu na Nyuki, ilete tija kwa taifa.

Katika ufunguzi huo, alizindua mipango miwili kabambe ya kitaifa ukiwemo Mpango wa tatu wa Kitaifa wa Utafiti wa Misitu wa mwaka 2021-2031 na Mpango wa Kwanza wa Utafiti wa Ufugaji Nyuki wa mwaka 2020-2030.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tafori, Dk Revocatus Mshunguzi alisema lengo la kongamano hilo ni kujadili matumizi hafifu ya fursa za misitu nchini, kuchambua tafiti, sera na sheria kuhusu mnyororo wa thamani wa mazao ya misitu na nyuki.

BENKI ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imepongeza uthubutu ...

foto
Mwandishi: Gloria Tesha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi