loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Profesa Ndulu kuzikwa leo Dar

VILIO na huzuni vimetawala wakati mwili wa Gavana wa zamani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu ulipofi kishwa nyumbani kwake Mbweni, Dar es Salaam.

Mwili wa Profesa Ndulu ulifikishwa nyumbani hapo jana saa 8 mchana kutoka Hospitali ya Kumbukumbu ya Chuo Kikuu cha Hurbert Kairuki jijini Dar es Salaaam.

Mamia ya waombolezaji wakiwemo wanafamilia, waliupokea na kuendelea na maandalizi ya maziko, yatakayofanyika leo katika makaburi ya familia Kinondoni, Dar es Salaaam.

Msemaji wa Familia, mdogo wa marehemu, Exaudi Ndulu alilieleza HabariLEO kuwa Profesa Ndulu alitoa utaratibu wa wapi atazikwa siku akifariki dunia.

Huku akionesha risiti za mauzo ya maeneo mawili kutoka katika Halmashauri ya Kinondoni ya mwaka 1988, Msemaji huyo alisema Profesa Ndulu alinunua maeneo mawili katika Halmashauri ya Kinondoni mwaka 1988, ambako eneo moja alitaka azikwe siku akiaga dunia na eneo lingine atakapozikwa mama yake mzazi.

Exaudi alisema mama yao alifariki dunia mwaka 2011 na kuzikwa katika eneo aliloandaliwa na mwanawe huyo ; na eneo lililobaki ndilo atakapozikwa Profesa Ndulu. Profesa Ndulu aliaga dunia Jumatatu wiki hii katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki jijini Dar es Salaam.

Profesa Ndulu aliwahi kuwa Naibu Gavana wa BoT mwaka 2007-2008 na baadaye Gavana kuanzia Januari mwaka 2008 hadi Januari 2018. Marehemu ameacha mke, watoto watatu, na wajukuu wawili.

foto
Mwandishi: Na Selemani Nzaro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi