loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ndalichako aagiza somo la Historia liwe na mvuto

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako ameitaka Taasisi ya Elimu Tanzania kukusanya maoni yanayotolewa kuhusu somo la Historia ya Tanzania na iyachambue ili somo hilo liwe na mvuto.

Profesa Ndalichako alisema taasisi ikifanya hivyo, itaongeza ari ya kulisoma somo huio ili wanafunzi waipende nchi yao. Aliyasema hayo jana alipofungua mkutano wa wadau kuhusu kupokea maoni juu ya maudhui ya somo la Historia Tanzania jijini Dar es Salaam.

Profesa Ndalichako alisema baada ya kupokea maoni ya wadau, taasisi itayafanyia kazi na kuhakikisha kuwa yanaingizwa katika mihutasari na vitabu vya somo hilo.

“Kazi hii hakuna kulala, mnapaswa kuifanya usiku na mchana ili mfanyie kazi maoni ya wadau...ninasisitiza kuwa kazi ya kukamilisha uandishi wa vitabu ikamilike mwezi wa tatu kama ilivyopangwa ili uchapaji na usambazaji ukamilike kabla ya mwezi Julai ambapo somo hili litaanza kufundishwa rasmi.

Mwenyekiti wa baraza simamia utekelezaji wa ukamilishwaji wa kazi hii,” alisema. Profesa Ndalichako alisema taasisi hiyo imekamilisha kazi ya kuandaa rasimu za muhtasari wa somo la Historia ya Tanzania itakayotumika kuanzia elimu ya awali, msingi na sekondari hadi kidato cha sita.

“Kama ambavyo imekuwa ikisisitizwa na Mheshimiwa Rais, lengo la kuanzishwa kwa somo la Historia ya Tanzania ni kuamsha na kujenga moyo wa uzalendo kwa kuwafanya Watanzania kuifahamu nchi yao, kuithamini, kuipenda na kulinda rasilimali zake,” alisema. Alisema historia ya Tanzania, itasaidia pia wanafunzi kutambua harakati za kimaendeleo zinazoendelea nchini.

Profesa Ndalichako alisema Tanzania ni nchi yenye mchango mkubwa katika harakati za ukombozi wa Afrika, kwani kambi za wapigania uhuru wa nchi za Afrika ya Kusini, Msumbiji na Namibia, zilikuwa nchini wakati wa kudai uhuru hadi kupata Uhuru.

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi