loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mourinho amfagilia Dele Alli

JOSE Mourinho amempongeza Dele Alli kwa kiwango kizuri alichoonesha baada ya kufunga bao kwenye mechi ligi ya Europa ambayo Tottenham ilishinda mabao 4-0 dhidi ya Wolfsberger juzi.

Jose Mourinho alisema inafurahisha kuona Dele Alli amerejea akiwa kwenye kiwango kizuri baada ya kufunga bao moja na kutengeneza mawili. 

Alli alifunga bao la ufunguzi dakika ya 10 na kisha akatoa pasi ya mabao yaliyofungwa na Carlos Vinicius, na kisha Gareth Bale akafunga la nne na kuifanya Spurs kutinga hatua ya 16 kwa ushindi wa jumla ya mabao 8-1 dhidi ya timu hiyo ya Austria.

Msimu huu umekuwa mgumu kwa Alli, baada ya kuachwa nje ya Mourinho, lakini alikuwa na mechi nzuri katika mechi hiyo akicheza baada ya kushindwa kuondoka kwenye usajili wa Januari.
Kuna baadhi ya madai kwamba wamecheza dhidi ya timu ndogo kwenye michuano hiyo ya Ulaya lakini ni hatua kubwa na Mourinho ameifurahia. 

"Bao ambalo sihitaji kulizungumzia kwasababu kila mmoja ameliona na naamini ni duniani kote na runinga zote za michezo watu watatizama, aihitaji kulizungumzia,” alisema Mourinho.

"Kwangu ubora wa kiwango aliouonesha ndio jambo muhimu, amecheza vizuri sana.”

"Ni kweli hayuko vizuri,  unaweza kuhisi hilo kupitia kiwango chake katika mechi ya kwanza kuanzia dakika ya 55-60 alikuwa chini, hilo ni jambo la kawaida kwenye mechezaji aliyetoka kwenye majeraha.”

"Lakini kwa wakati huu tunaokwenda kucheza kila baada ya siku tatu, mechi 10 Machi, kuwa na Dele katika kiwango chake, inafurahisha.”
"Lakini sijasema ni Dele tu (Harry) Winks, (Moussa) Sissoko, kuwa nao kikosini ni jambo zuri.”

K

IUNGO wa Manchester United, Paul Pogba ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi