loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kumbilamoto, Meya mpya jiji la Dar es Salaam

Rais John Magufuli amesema Manispaa ya Ilala imepandishwa hadhi kuwa Jiji la Dar es Salaam na kwamba aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto ndiye Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, na Naibu Meya wa Ilala naye amepandishwa hadhi kuwa Naibu Meya wa jiji hilo.

Rais Magufuli amesema kuwa hatua hiyo imefuata vigezo na kusisitiza kuwa Ilala wanastahili na ni haki yao wala hawajapendelewa na kuanzia sasa bajeti yao itaongezeka.

Hatua hiyo imekuja baada ya jana, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala wa Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo kutekeleza maagizo ya Rais Magufuli ya kulivunja Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na kuipandisha hadhi Halmashauri ya ya Manispaa ya Ilala kuwa jiji la Dar es Salaam kuanzia Februari 24, mwaka huu.

Akizungumza baada ya kuweja jiwe la msingi la Soko la Kisasa la Kisutu leo jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli alisema Manispaa ya Ilala ina hadhi ya kuwa jiji kwa sababu ina sifo zote ikiwemo kuongoza kwa ukusanyanji mapato ukilinganisha na halmashauri nyingine zote.

foto
Mwandishi: Mwandishi wetu 

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi