loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Barrick wekezeni bila uwoga- Waziri Biteko

WAZIRI wa Madini,Dotto Biteko amesema kampuni ya uchimbaji wa madini ya Barrick Gold mine inatakiwa kuwekeza bila kuogopa chochote bali ihakikishe inazingatia sheria za madini pamoja na sheria za nchi.

Dk Biteko alisema hayo wakati alipokuwa katika mkutano malumu na watendaji wa mgodi wa Barrick.

‘’Nachowambia Barrick wahakikishe,wanawekeza nchini kwetu kwa kuzingatia sheria zetu za madini tulizoboresha pamoja na sheria za nchi. Rais wetu amewahakikishia ushirikiano’’ alisema Biteko.

Biteko alisema mpaka sasa mgodi huo umeshatoa ajira zaidi ya 42,000 kwa watanzania. Ameipongeza mgodi huo kwa kuendelea kufanya kazi na nchi yetu.

Alisema mgodi huo umewaweza kutoa dola ya marekani zaidi ya milioni 290 kwa malipo mbali mbali katika kampuni zetu za ndani.

Mkurugenzi Mtendaji wa mgodi Barrick, Mark Bristow alisema wataendelea kufanya kazi zao za uchimbaji katika migodi ya (North Mara, Bulyanhulu and Buzwagi) kwa kuendelea kufuata utaratibu wote na sheria za nchi.

 Alisema wamekuwa wakishirikiana na jamii za mitaa kurejesha leseni ya kijamii ya migodi kufanya kazi na tunashirikiana kwa karibu na mamlaka kushughulikia masuala ya mazingira huko North Mara.

Alisema, wanafanya kazi kwenye mkakati wa wasambazaji wa ndani na vile vile mpango wa maendeleo ya jamii ili kuunda fursa endelevu za kiuchumi kwa watu walio karibu na migodi yetu . Alisema wamefanikiwa kutoa gawio la mpito la fedha dola za kimarekeani milioni 250 na walilipa Oktoba 2020.
 

foto
Mwandishi: Alexander Sanga,Mwanza

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi