loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kongole Namungo kwa kutinga makundi Afrika

WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho la Afrika Namungo FC sasa ni rasmi wanashiriki hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Timu hiyo ilijihakikishia nafasi hiyo baada ya kupata ushidi wa jumla wa mabao 7-5 katika mechi mbili zilizochezwa  kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo wa kwanza, Namungo ilishida mabao 6-2 kabla ya Alhamisi kufungwa 3-1 na hivyo kusonga mbele kwa jumla ya mabao 7-5.

Namungo huu ni msimu wake wa pili kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara tangu ilipopanda kutoka Daraja la Kwanza na ni mara ya kwanza  kushiriki michuano ya kimataifa.

Tunapenda kuipongeza Namungo kwa kufuzu kwa hatua ya makundi na huu ni mfano mzuri kwa timu zingine ambazo zimekuwa zikishiriki Ligi Kuu Tanzania Bara kwa muda mrefu huku nyingine zikiwa na kazi ya kupambana zishuke daraja na zingine zikipambana ili kuendelea kuwepo katika ligi hiyo kila msimu.

Namungo vizuri mmeingia katika historia ya soka la Tanzania na Afrika, lakini hatua inayofuata ni ngumu na mna nafasi ya kuendelea kuweka rekodi katika soka kwa kufika mbali zaidi.

Hiki ni kipindi chenu kuendelea kuweka historia, hivyo mna nafasi ya kufanya usajili ili kuboresha kikosi chenu tayari kwa hatua hiyo ya makundi, ambapo mmepangwa Kundi D pamoja na Raja Casablanca ya Morocco, Nkana ya Zambia na Pyramids ya Misri.

Ni kweli mmepangwa na timu zenye uzoefu mkubwa katika soka la Afrika lakini hiyo isiwatishe kwani bado mna nafasi ya kuendelea kufanya vizuri katika michuano hiyo ya pili kwa ukubwa kwa klabu Afrika.

Ni matarajio yetu mtajiandaa vizuri na watanzania tuko nyuma yenu kuwasapoti mwanzo hadi mwisho mtakapokuwa mkishiriki mashindano hayo.

Katika soka hakuna lisilowezekana, hivyo kikubwa ni kujipanga vizuri kwa kiwango kile cha michuano ya Afrika na hasa baada ya kujua mtacheza na nani katika hatua hiyo ya makundi.

Baada ya kufuzu kwa hatua hiyo, sasa kilichobaki katika kipindi hiki kifupi ni kutumia vizuri nafasi 10 za usajili zilizotolewa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf) ili timu zijiimarishe katika kipindi hiki kigumu cha janga la corona.

Hongera Namungo na tunawatakia kila la kheri katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

 

Swali: Nia ya kufunga ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi