loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Hekta 618 zanyunyiziwa viuatilifu kuua Nzige

WANANCHI  wa Wilaya ya Siha, Mkoa wa Kilimanjaro wameipongeza serikali kwa hatua iliyochukua kudhibiti makundi ya nzige waliovamia maeneo ya mashamba yao hivi karibuni.

Wakizungumza na waandishi wa habari, baadhi ya wakulima  walimweleza Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe aliyetembela mashamba ya Nanai eneo la Sanya Juu wilaya ya Siha kwamba kasi ya serikali imewapa moyo mkubwa.

Serikali kwa kutumia  ndege imekuwa kwa siku tatu mfululizo inapambana na nzige wa jangwani kwa kuwanywesha viuatilifu kwa njia ya ndege na mkononi. Mpaka jana serikali imenyunyiza dawa hekta 618 katika maeneo ya Longido (390), Sinha (38), Ildonyo na Kikokouwa (65), Simanjiro (35) na Siha (90).

Mkulima na mmiliki wa shamba la Kafori West Kilimanjaro, Felix Mosha alisema tukio la kuvamiwa na nzige juzi lilileta taharuki kwa wakazi wa maeneo hayo kwa kuwa sasa ndio wameanza kupanda mazao mashambani lakini wamefarijika kuona hatua za serikali chini ya Wizara ya Kilimo kuwadhibiti  nzige  hao.

“Tunaishukuru serikali kwa kuja kwa haraka, leo tumeona wataalamu wamefanikiwa kuwaangamiza nzige waliovamia mashamba yetu ya makademia na ngano  yanaendelea kuwa salama,” alisema Mosha.

Mkulima Hassan Gonga anayemiliki shamba la Nanai, Wilaya ya Siha, alisema mara baada ya wadudu hao kuvamia shamba lake la makademia, waliwatafiti wadudu hao na kugundua kuwa hawapendi kelele hivyo wakaweka vifaa vya kupiga kelele shambani hapo hali iliyosababisha nzige hao waondoke kwenda msituni na kuliacha shamba likiwa salama bila madhara.

Akizungumzia operesheni ya kuangamiza nzige, Naibu Waziri Kilimo Bashe alisema kazi ya kuangamiza nzige tangu walipovamia maeneo ya Tanzania inaendelea vizuri na wadudu wamedhibitiwa kwa kupuliziwa viuatilifu kuwaua  kwa njia ya ndege na mabomba ya kushikwa kwa mikono.

Bashe alisema  kuwa wizara inatambua wilaya ya Siha ni muhimu kwa kilimo hivyo lazima itazamwe kwa karibu nzige wasije haribu ndio maana wanaendelea kwenda kujionea kazi ya kuwadhibiti nzige hao ambapo ameshuhudia makundi ya nzige waliokufa baada ya kupuliziwa sumu.

Aliongeza kusema wizara imeongeza vifaa vya kusaidia kupambana na nzige pia imeanzisha mafunzo kwa maafisa ugani wa vijiji na kata kutambua aina za nzige ili iwe rahisi kudhibiti pale watakapojitokeza kwenye maeneo yao

“Mpaka sasa Longido tumefanikiwa kwa asilimia 95 kazi hiyo imefanikiwa hakina masalia ya nzige waliovamia Siha walitokea Longido baada ya kundi lao kupuliziwa sumu  hivyo wakakimbia na sasa tumewafuata hapa Sanya Juu tumewaua” alisema.

Bashe aliongeza kusema kazi ya kudhibiti nzige wilaya ya Simanjiro imeenda vizuri ambapo hadi sasa taarifa za wataalamu zinaonesha kumebakia kundi moja lililolojificha kwenye milima na kazi ya kulifuatilia ili liangamizwe.

“Hadi sasa hakuna madhara yoyote kwenye mazao ya wakulima tangu nzige wavamie Januari mwanzoni. Ni heri tupate madhara ya kufa kuku lakini nzige lazima tuwatafute kokote waliko,” alisisitiza Waziri Mkenda.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia za visumbufu Taasisi ya Udhibiti wa Viautilifu kwenye Ukanda ywa Kitropiki (TPRI) Julius Mkenda alieleza kuwa kundi la nzige lililovamia wilaya ya Siha ni baadhi ya waliokimbia Longido baada ya kazi ya kunyunyizia kiuatilifu Februari 22, 2021 hivyo wakatoroka na kuingia Siha na kuwa siyo kundi jipya kwa mujibu wa utafiti waliofanya.

Mkenda alibainisha kuwa nzige waliovamia Siha wanaendelea kuangamizwa kwa kutumia ndege maalumu pia mabomba ya kupuliza kwa mikono kwa wale walio jirani na makazi ya watu  ambapo zoezi limeenda vema jana na leo na kuwa wataendelea kuchukua hatua za kuwadhibiti .

Waziri wa Kilimo pamoja na Naibu Waziri wa Kilimo wapo kwenye mikoa ya Arusha na Kilimanjaro kufanya ufuatiliaji wa karibu wa udhibiti wa makundi ya nzige ili wasije haribu mashamba ya wakulima.

JOPO la Majaji 12 nchini Marekani limemtia hatiani ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Siha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi