loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ulanga wajipanga kuzalisha karangamiti kwa wingi

SERIKALI wilaya ya Ulanga ,mkoani Morogoro imejipanga kuwezesha wakulima kuingia kwenye kilimo cha uzalishaji wa karangamiti (macademia) kwa wingi na kuiwezesha wilaya hiyo kufahamika kwa zao hilo Afrika Mashariki na Kati.

Katika hatua  hiyo serikali ya wilaya hiyo tayari imetenga  jumla ya ekari 9,025 kwa ajili ya kilimo cha karangamiti na kumilikishwa wananchi.

Mkuu wa wilaya  ya Ulanga,  Ngollo Malenya alisema hayo  hivi karibuni mjini Mahenge alipokuwa ameupokea  ujumbe wa  Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB ).

Ujumbe wa TADB uliongozwa na Mkurugenzi Mtendaji,  Japhet Justine na  ulikuwa na lengo la  kuona  namna wilaya ya Ulanga inavyoweza kuwekeza na kunufaika na kilimo cha karangamti .

Malenya alisema  wilaya hiyo  ina ardhi yenye rutuba na hali ya hewa inayowezesha zao la karangamiti kustawi vizuri na imetenga  ekari hizo  kwa ajili ya kilimo hicho.

Malenya alisema mradi  wa karangamiti unatarajiwa kuwa moja ya miradi mikubwa na wa kipekee kwa Afrika Mashariki na kati.

Hata hivyo baada ya kushiriki kikao hicho ujumbe kutoka TADB ulitembelea shamba la karanga miti linalomilikiwa na kampuni ya Tanzania Nuts Limited .

Mkuu huyo wa wilaya hiyo na ujumbe wake waliweza kuona uzalishaji wa miche ya karangamiti na shamba la karanga miti na kuweza kujifunza namna miche ya karanga miti inavyoandaliwa hadi wakati wakupanda.

Baada ya kutembelea  shamba la kampuni hiyo mkuu wa wilaya hiyo alisema, “tumejipanga na tuko tayari kuifungua wilaya yetu na tunataka tufahamike duniani kwa kuzalisha karanga miti.”

Ofisa  Ushirika wa halmashauri ya wilaya hiyo, Charles Eman kwenye taarifa yake ya namna wananchi  wanavyoshiriki katika mchakato wa kuanza kilimo cha karangamiti alisema wameamua kuwajengea uelewa wa ushirika na manufaa ya kwa kuwa  kwenye ushirika.

Kwa upande wake  Mkurugenzi Mtendaji, Japhet alisema  TADB ni jukumu lake kuchagiza kilimo nchini na kwenye wilaya ya Ulanga benki hiyo ipo  tayari kuwekeza kwa wakulima wetu.

Japhet alisema kwa  kutambua hilo, TADB inadhamiria kuwawezesha wakulima wa Ulanga sio tu kwa mtaji bali pia kwa kuweka ofisa kilimo atakayesimamia na kuwashauri wakulima kwa kilimo chenye tija.

Mkurugenzi Mtendaji huyo alisema, “hii inahamasisha vijana kufahamu kuwa kilimo kinahitaji uvumilivu ilikuweza kufanikiwa, ni wakati sasa vijana kubadili fikra na kuelewa kuwa fursa zipo shambani.”

Karanga miti ni zao linalotajwa kuwa na faida mbalimbali na virutubisho vingi muhimu kwa mwanadamu.

JOPO la Majaji 12 nchini Marekani limemtia hatiani ...

foto
Mwandishi: John Nditi, Morogoro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi