loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ahimiza maombi apatikane Makamu wa Kwanza wa Rais Z’bar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi amewaomba waumini wa dini ya Kiislamu kuendelea kumuomba Mwenyezi Mungu apatikane Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar mwenye nia njema na dhamira njema kama Maalim Seif Sharif Hamad.

Alisema hayo jana baada ya sala ya Ijumaa katika Msikiti Raudhwa uliopo Darajabovu madukani, Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi.

Akitoa salamu kwa waumini wa msikiti huo, Dk Mwinyi alisema Wazanzibari wote wanahuzunika kwa kuondokewa na kiongozi wao mahiri, Maalim Seif hivyo ni vyema wakamuombea dua popote pale walipo.

Alisema alishiriki kikamilifu katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa, ambayo imeleta maridhiano na kuwezesha Zanzibar kuwa ya amani, yenye umoja na mshikamano.

Alisema maridhiano yameimarisha umoja, amani na mshikamano ambapo hapo mwanzo vitu hivyo havikuwepo, kwani wananchi walikuwa wameshapotea, lakini Mwenyezi Mungu ameleta rehema zake hizo.

Alisema kwamba Zanzibar ilipo ni pazuri na Wazanzibari ni wamoja.

Alisema zamani waumini walikuwa wakichagua misikiti ya kusali, lakini sasa wanasali pamoja. Alisema kuna kila sababu ya kuendeleza hali ya umoja, amani na mshikamano, kwani Mwenyezi Mungu ameshawaweka Wazanzibari kwenye mstari na ni vyema hali hiyo ikaendelezwa kwa manufaa ya wananchi wote.

Alimshukuru mfadhili aliyemalizia ujenzi wa msikiti huo ambao waumini wake walimuomba Rais afanikishe hilo alipokwenda kusali Januari 8, mwaka huu. Mfadhili huyo alijitokeza na kumwambia kwamba amuachie aifanye kazi hiyo.

Kwa mujibu wa Dk Mwinyi, Maalim Seif ndiye alimpa ujumbe kwamba waumini wa msikiti huo wanataka kusali pamoja naye ili wamueleze matatizo yao na ndipo akatekeleza ombi hilo na waumini hao kumuomba kumalizia msikiti huo. Akitoa hotuba ya sala ya Ijumaa, Shehe Ali Fakih Abdallah alisisitiza haja ya kukatazana mabaya na kuelekezana mazuri.

Alisema sifa za wenye akili ni wale wenye kutekeleza ahadi, ambazo wamekua wakiziahidi na hawaendi kinyume na ahadi hizo walizoziahidi.

Wakati huo huo, Dk Mwinyi alifika nyumbani kwa mjane wa Maalim Seif katika eneo la Mbweni na kuonana naye pamoja na familia yake. Alimuahidi kuendelea kushirikiana naye wakati wote yeye pamoja na serikali anayoiongoza.

JOPO la Majaji 12 nchini Marekani limemtia hatiani ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi