loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Lukuvi akabidhi eneo Ubungo aliloagiza JPM

WIZARA ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imekabidhi ardhi yenye ukubwa wa ekari 52 kwa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli, lililotokana na ombi la mbunge wa Kibamba, Issa Mtemvu.

Rais Magufuli alitoa agizo hilo hivi karibuni alipokuwa akizindua Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli mkoani Dar es Salaam baada ya Mtemvu kumuomba ardhi hiyo kwa lengo la kuifanyia matumizi ya kijamii.

Alitoa siku tatu kwa wizara kukamilisha hati ya ardhi hiyo na kuikabidhi kwa halmashauri.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alikabidhi hati hiyo katika ofisi za Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mtemvu alithibitisha kukabidhiwa eneo hilo la Njeteni lililo katika Kata ya Kwembe na kueleza shughuli ambazo wanatarajia kuziendesha.

“Pamoja na kwamba Manispaa ya Ubungo imeshalipata eneo hilo kutoka wizarani, mimi nina jukumu la kuhakikisha kuwa matumizi ya eneo hilo yanakuwa mazuri kama yalivyopagwa na Manispaa kabla ya kulipata,,” alisema Mtemvu.

Alitaja malengo ya manispaa katika eneo hilo kuwa ni pamoja na kujenga Kituo cha Afya cha Kwembe ambacho kitakuwa cha kwanza katika kata hiyo katika historia, kwani mpaka sasa eneo hilo halina zahanati.

“Kati ya vituo vitatu vinavyotarajiwa kujengwa katika Wilaya ya Ubungo mwaka huu wa fedha, viwili vitajengwa katika Jimbo la Kibamba ambapo kimojawapo kitajengwa katika Kata ya Kwembe katika eneo hilo,” alisema Mtemvu.

Mtemvu alisema malengo mengine ya Manispaa ya Ubungo ni ujenzi wa Shule ya Msingi ya Kwembe itakayokuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi wa eneo la Njeteni na maeneo jirani.

Alisema malengo mengine yanatokana na matakwa ya mbunge, ambayo ni ujenzi wa Kituo cha Michezo alichokiita Sports Arena, kitakachoshirikisha michezo mbalimbali kwa ajili ya kujenga afya za wananchi.

Alisema wananchi wanahitaji huduma mbalimbali zikiwamo masoko na eneo la maziko.

Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Ubungo, Beatrice Dominic alikiri kupokea hati ya eneo hilo kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Hata hivyo hakufafanua zaidi kuhusu mipango ya utekelezaji mpango katika eneo hilo.

JOPO la Majaji 12 nchini Marekani limemtia hatiani ...

foto
Mwandishi: Selemani Nzaro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi