loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wizara ya habari yaanza kutekeleza agizo la Rais Magufuli

Katibu Mkuu Wizara ya  Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Hassan Abbasi amebainisha kuwa Wizara hiyo imeanza kwa kasi kutekeleza agizo la Rais Dk John Pombe Magufuli  lililotaka utoaji wa   taarifa za Serikali kwa umma.
 

Dk Abbasi ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali amebainisha hayo leo mkoani Morogoro alipokuwa akitoa mada kwenye Semina ya Wahariri Kuhusu Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere.

Amesema kuwa Waziri wa Wizara hiyo, Innocent Bashungwa tayari amesaini barua yenye maelekezo hayo kuzijulisha taasisi zote za umma kuhusiana na hilo na ofisi yoyote itakayokaidi agizo hilo isitafute wa kumlaumu. 

 “Utoaji wa habari kwa umma ni jambo la kisheria na kikatiba na maelekezo ya muheshimiwa Rais ni sahihi atakayekaidi agizo hilo amekaidi mamlaka, amekaidi sheria na amekaidi katiba” amesema Dk Abbasi.

JOPO la Majaji 12 nchini Marekani limemtia hatiani ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi