loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kiwanda chapongezwa kuwekeza katika mawasiliano

NAIBU Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Kundo Mathew, amekipongeza Kiwanda cha Raddy Fibre Solution cha Mkuranga mkoani Pwani kwa kuwekeza katika sekta ya mawasiliano.

Akizungumza na wananchi wa wilaya hiyo jana baada ya kukagua uzalishaji wa bidhaa za mkongo wa taifa unaofungwa na kiwanda hicho cha wazawa, Kundo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bariadi, alisema uwekezaji huo uliogharimu Sh bilioni 1.7 utafanikisha ujenzi wa mkongo wa taifa upunguze gharama na kuokoa fedha za kigeni.

Mathew alizitaka Idara za Uhamiaji na Zimamoto kushirikiana na wawekezaji hao kutimiza malengo yao kwani kiwanda hicho kinalenga kutoa ajira zisizopungua 400 sambamba na kuongeza mapato ya halmashauri ya wilaya na Serikali Kuu.

Mkurugenzi wa Kiwanda cha Raddy Fibre Solution, Ramadhani Mlanzi, aliipongeza serikali kwa kuwezesha kuanza kwa ujenzi, huku akiweka bayana azma ya kutengeza ‘cable za fibre’ za kilometa 24,000 kwa mwaka na kuongeza wao ni kati ya nchi tatu pekee za Afrika zinazofanya uzalishaji huo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Mshamu Munde, alisema katika taarifa ya halmashauri kuwa, mazingira rafiki kwa uwekezaji ikiwemo ardhi ya kutosha yamevuta zaidi ya wawekezaji 80 hali iliyochangia kutoa ajira kwa wananchi na kupaisha mapato.

Akiwasilisha taarifa ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mkuu wa Uendeshaji, Albert Richard, alisema wametumia Sh bilioni 161 za serikali kujenga mikongo katika kata 1057 nchini huku katika Wilaya ya Mkuranga wakitumia Sh milioni 200.

Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga, aliwataka wajenzi wa mikongo kutoa taarifa kwa mkurugenzi, uongozi wa kata na vijiji ili kujiridhisha kiusalama.

 

JOPO la Majaji 12 nchini Marekani limemtia hatiani ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalum, Mkuranga

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi