loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tunaomba ‘viatu’ vya Kijazi vimtoshe Dk Bashiru

LEO tunaanza Maoni Yetu tukisema: “Japo tunaomba ‘viatu’ vya Kijazi ‘vimtoshe’ Dk Bashiru Ally Kakurwa, tunaamini vitamtosha kwa kuwa alishaonesha dalili na uteuzi umefanywa na iongozi mkuu na makini wa kitaifa, Rais John Magufuli.”

Itakumbukwa kuwa, juzi Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais (Ikulu) ilitoa taarifa ikisema Rais Magufuli amemteua Dk Bashiru kuwa Katibu Mkuu Kiongozi na pia akamteua kuwa balozi. Aliapishwa jana.

Rais alimteua Dk Bashiru kuwa Katibu Mkuu Kiongozi kuchukua nafasi iliyoachwa na Balozi John Kijazi aliyefariki dunia Februari 17, mwaka huu katika Hospitali ya Benjamin Mkpa iliyopo Dodoma alipokuwa akipatiwa matibabu.

Kabla ya kuteuliwa kutumikia Watanzania katika wadhifa huu mpya na mkubwa kitaifa, Dk Bashiru alikuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) tangu Mei 2018, alipoteuliwa kumrithi Abdulahman Kinana.

Sisi tunampongeza Dk Bashiru kwa utumishi wake uliotukuka kwa Watanzania kiasi cha kumfanya kuteiliwa zaidi ili apanue wigo wa utumishi wake kwa Watanzania.

Tunampngeza tukisema hayo kwa kuwa tunajua kabla ya kuwa Katibu Mkuu wa CCM, Bashiru alikuwa akiwatumikia Watanzania kupitia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) alipokuwa Mhadhiri Mwanadamizi katika Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala.

Tunasema, utumishi wake katika kuandaa wasomi wa Tanzania akiwa UDSM na namna alivyoonesha umahiri katika fani ya sayansi ya siasa na utawala, ndiyo mambo yaliyomuanika hata CCM wakamuona na kumtaka awatumikie kwa ngazi ya kitaifa kama katibu mkuu.

Bado tunampongeza kwa kuwa utumishi wake akiwa katika chama kimoja pia umeonesha kututuka hadi Rais kuona sasa anafaa kuwatumikia Watanzania wote; wa dini na vyama vyote kama Katibu Mkuu Kiongozi kwani ameonesha hekima, maadili, utu, uadilifu na hasa uwezo wa kuwatumikia Watanzania.

Ndiyo maana tunasema, tunamtakia kila la heri katika utumishi mpya kwa wadhifa wa Katibu Mkuu Kiongozi huku pia sasa akiwa na hadhi ya balozi.

Tunasema, hongera Dk Bashiru wape Watanzania utumishi uliotukuka ama iwe kwa wakati unaofaa, au wakati usiofaa ukitamba kuwa, Rais Magufuli kwa niaba ya Watanzania, amekuteua akiwa na imani kubwa na utumishi wako, hivyo ana matarajio kadhaa kwako.

Tunaamini kupitia juhudi na maarifa uliyo nayo, uadilifu na kumtanguliza Mungu kwa kila jambo, utavaa viatu vya mtangulizi wako ambaye sasa anapumzika mbele ya Kiti cha haki na vitakutosha.

Sisi tunasema, chunguza na kujifunza mema aliyoyafanya au aliyotaka kuyafanya mtangulizi wako, ili uyaendeleze kwa ubora zaidi.

Sisi tunakuombea utumishi mwema tukisema, ukiweka juhudi za kuvaa viatu vya kijazi kiutendaji, kiuadilifu na hata kiweledi na utu kama ulivyoapa, ukimshauri kwa hekima rais, utakidhi maratajio ya Rais Magufuli aliyekuamini kwa niaba ya Watanzania

Swali: Nia ya kufunga ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi