WANACHAMA wa Chama cha Republican nchini Marekani, wanaanza mkutano wao wa kila mwaka leo, ambao Rais wa zamani, Donald Trump anatarajiwa kuhutubia.
Mkutano huo utawakusanya watu mashuhuri wa chama hicho. Unafanyika kukiwa na swali muhimu juu ya kama Trump atagombea tena katika uchaguzi mkuu ujao, utakaofanyika baada ya miaka minne.
Miongoni mwa wanaotarajiwa kuhudhuria mkutano huo utakaofanyika mjini Orlando huko Florida ni wanasiasa maarufu wa chama hicho, wakiwemo maseneta Ted Cruz, Tom Cotton na Josh Hawley.
Wengine ni wabunge wa Baraza la Wawakilishi, Steve na Matt Gaetz. Wote hao ni miongoni mwa watu wa karibu wa Trump.