loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ujenzi kituo kibwa cha polisi Mloka waanza

UJENZI wa kituo cha polisi katika eneo la Mloka wilayani Rufiji umeamza ukiwa ni sehemu ya mikakati ya kuimarisha ulinzi katika Mradi wa Kufua Umeme wa Mwalimu Julius Nyerere.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo alibainisha hayo alipokuwa akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene aliyetembelea ofisini kwake.

Alisema kituo cha polisi kilichopo kipo mbali, hivyo ipo haja ya kujenga kingine karibu na eneo la mradi ili kuimarisha ulinzi katika mradi huo mkubwa na wenye manufaa makubwa kwa taifa.

"Michoro ya jengo ilishaandaliwa tena ya daraja ‘A’ haiwezekani tukawekeza fedha nyingi tukaacha kuimarisha ulinzi. … Ujenzi wa bwawa hilo ni vema uende sambamba na ujenzi wa kituo kikubwa cha polisi," alisema Ndikilo.

Alisema mkoa pia unaendelea kupambana na biashara za magendo zinazoshamiri kutokana na kuwapo kwa mwambao wa Bahari ya Hindi ambapo kuna bandari bubu nyingi.

"Suala la ukamataji wa bidhaa za magendo linapaswa kwenda pamoja na ushirikwishaji wa taasisi nyingine pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),” alisema Ndikolo.

Akaongeza: “Kwa mfano, polisi wanaweza kukamata madumu ya mafuta ya kupikia kwa kukosekana kwa nyaraka muhimu, lakini kesho yake unashangaa mzigo uliokamatwa unazo nyaraka zote sasa unashangaa zimetoka wapi, hivyo ni vema kila taasisi kutimiza wajibu ipasavyo."

Alisema changamoto nyingine iliyopo mkoani hapa ni migogoro ya ardhi ambayo mingi imetokana na ardhi ya Pwani kupanda thamani.

Alitaka Jeshi la Polisi liendelee kushughulikia migogoro hiyo inapogundulika kuwapo jinai ndani yake ili kusaidia baraza la ardhi na kupatikana kwa haki kwa wakati.

"Tunaishukuru Wizara ya Mambo ya Ndani kupitia Jeshi la Polisi kwa kuendelea kuimarisha usalama wa wawekezaji na miradi yao na mkoa utaendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kulinda miradi ya wawekezaji," alisema Ndikilo.

foto
Mwandishi: John Gagarini, Kibaha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi