loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Gomes atuma salamu JKT

KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes, amesema ushindi katika mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam (FA) ni mzuri kuelekea katika mchezo  wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya JKT Tanzania.

Akizungumza Dar es Salaam baada ya mchezo huo Gomes alisema ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya African Lyon na kutinga 16 bora unawapa hamasa ya kwenda kufanya vizuri katika mchezo huo utakaochezwa kesho Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

 “Tumefurahi kushinda mchezo huu na ni nzuri kwa ajili ya michezo yetu ijayo, Jumatatu (kesho) tuna mchezo muhimu dhidi ya JKT nao tunahitaji kushinda kutimiza malengo yetu ya kuongoza ligi,” alisema.

Kocha huyo alisema kwa kutambua umuhimu wa mechi zijazo ukiwemo wa kesho na ule wa kimataifa dhidi ya El Merreikh aliamua kuwapumzisha baadhi ya wachezaji wa kikosi cha kwanza ili wapate nguvu.

Alisema moja ya malengo yao kwenye ligi ni kuongoza na kutetea taji lao na kimataifa anajipanga kwenda kulinda nafasi yao kwa kuhakikisha wanapambana na kupata matokeo mazuri.

Katika hatua nyingine, Gomes alisema amevutiwa na kiwango cha mchezaji wake Perfect Chikwende.

Alisema alicheza vizuri katika mchezo dhidi ya Lyon na anaamini ataendelea kuwa hivyo, kulinda ubora wake.

Mbali na huyo alisema anamuombea John Bocco apone haraka kwani anamuhitaji katika michezo ijayo.

Wakati huo huo Simba imemrejesha kazini meneja Patrick Rweyemamu ambaye alisimamishwa kazi Ockoba, mwaka jana kwa tuhuma za kuihujumu klabu hiyo.

MSHAMBULIAJI wa Simba, Meddie Kagere, anamhofia ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi