loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Matokeo Coastal yamshtua Mgunda

KOCHA Mkuu wa Coastal Union, Juma Mgunda amesema haridhishwi na ameshtushwa na matokeo waliyopata hivi karibuni ya kupoteza mechi mbili mfululizo.

Coastal imepoteza michezo yake miwili dhidi ya Dodoma Jiji kwa kufungwa mabao 2-1 na JKT Tanzania kuwakandamiza mabao 2-0 katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

Lakini kabla ya mechi hizo mbili, Coastal ilifanikiwa kuifunga Azam mabao 2-1 ikiwa imeusubiri ushindi huo baada ya mechi tano mfululizo ambao ndio mchezo pekee ilioshinda katika mechi nane za mwisho walizocheza.

Mgunda alieleza matokeo hayo hayafurahishi ingawa yamekuwa yakimshtua kulingana na yanavyokuja mfululizo lakini hakuna budi zaidi ya kuendelea kupambana na kutafuta njia salama kukaa sawa.

“Ni jambo la kushtua kidogo na kutisha wakati mwingine maana matokeo siyo mazuri na yamekuwa yakija mfululizo lakini kuna wakati unagundua sisi ni wapambanaji na hii ni sehemu ya matokeo hivyo tunapaswa kukaa sawa na kuendelea kupambana.

“Kama kocha inanipasa kukaa na kuangalia nini cha kufanya katika wakati mgumu kama huu ili kuendelea na mechi zinazofuata tukiwa na mipango na mbinu imara za kujiweka sawa kwenye msimamo pia kwa kupata matokeo mazuri,” alisema Mgunda.

Kwa sasa Coastal yenye maskani yake mkoani Tanga, inashikilia nafasi ya 13 ikiwa na pointi 23 baada ya kucheza michezo 21.

Leo timu inacheza mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Ihefu katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi