loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Majaliwa kufanya ziara Katavi

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi ya situ tatu mkoani Katavi ambapo pia atazindua kitabu cha mwongozo wa uwekezaji katika mkoa huo.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Juma Homera amebainisha hayo leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mkoani humo.

RC Homera amesema Majaliwa atawasili mkoani humo Jumanne, ambapo baada ya ziara hiyo atazindua kitabu hicho.

Aidha, ameeleza kuwa viongozi wa serikali wa mkoa humo, wawekezaji na wadau watafanya ziara ya kutembelea maeneo ya uwekezaji na  vivutio vya utalii vilivyopo Ziwa Tanganyika na Hifadhi ya Taifa ya Katavi.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi