loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wizara kujenga maghala 24 kambi za JKT

WIZARA ya Kilimo itajenga maghala ya kuhifadhia mazao kwenye kambi 24 za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), ikianzia na Kambi ya Chita, Kilombero mkoani Morogoro.

Katika kambi hiyo pia kitajengwa kiwanda cha kuongeza thamani mpunga kabla ya kuuza.

Mkakati huo ulibainika wakati Katibu Mkuu wizara hiyo, Gerald Kusaya na Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Charles Mbuge waliposaini makubaliano ya ushirikiano wa miaka mitano katika masuala mbalimbali ukiwemo uzalishaji wa mazao kisayansi.

Kusaya alisema watashirikiana pia kufanya utafiti katika vituo 35 vya utafiti wa kilimo vikiwemo vikubwa 17 na vidogo 18 ili kuwezesha kilimo biashara.

Wizara hiyo na JKT pia watashirikiana kutumia na kusambaza teknolojia ya kilimo cha kisasa, kwa kuanzisha maeneo ya mfano katika uzalishaji wa kisasa, utumiaji pembejeo, mbegu, mbolea na uhifadhi kwa ajili ya wananchi wengi kujifunza na kutumia.

Kwa kuzingatia makubaliano hayo, pia JKT na wizara hiyo watashirikiana  kubadilishana taarifa za masoko ya ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kuuza mazao yaliyozalishwa na vijana kwenye vikosi vya JKT.

Aidha kila baada ya miaka mitano, watafanya tathmini ya ushirikiano kupitia kamati ya uongozi chini ya Katibu Mkuu wa Wizara na Mkuu wa JKT.

Kusaya alisema wizara inatamani kuona JKT inatimiza ndoto za kufanikisha shughuli zake. Alisema wizara hiyo italisaidia jeshi hilo kwa kuwa inaisimamia Tume ya Umwagiliaji, mitambo 57 ya kisasa ya kumwagilia, vituo vya utafiti na vyuo vya kufundisha maafisa ugani katika vyuo 14 nchini.

Alisema kwa kuwa JKT imejikita kuzalisha mazao, wanachangia kuendeleza uchumi na pato la taifa, wizara itahakikisha teknolojia bora ya mazao inasambazwa katika kambi kwa kutumia wataalamu.

"Itasaidia kuijengea uwezo JKT katika kusambaza teknolojia katika maeneo ya vipaumbele," alisema Kusaya. Alisema pia wizara itatoa huduma za umwagiliaji na kuhakikisha masoko yanapatikana kutokana na bidhaa zinazozalishwa.

Kwa mujibu wa Kusaya, wizara pia itasaidia kutoa huduma ya uhifadhi, kuongeza thamani mazao na utumiaji wa pembejeo katika uzalishaji.

Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Mbuge alisema jeshi hilo linapokea vijana wa kujitolea na kwamba tangu msimu wa 2019/2020 liliweka mkakati wa kuzalisha mahindi, mpunga na maharage na kuendesha kilimo cha umwagiliaji Chita, lakini wana changamoto ya maghala ya kuhifadhia mazao kwenye kila kikosi.

Alisema JKT pia ina changamoto ya uhaba wa rasilimali fedha katika kutekeleza azma ya kujenga maghala na kupanua kilimo zaidi hadi kufikia ekari 12,500.

Mwenyekiti wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Mkakati, Kanali Flassan Mabena alisema JKT ina mpango wa uzalishaji wa miaka mitano 2020/21 hadi 2024/25  wa kulima ekari 1,000 za mahindi katika Kambi ya Chita na makambi mengine 7,517 na kuwa na jumla ya ekari 8,517.

Pia inajiandaa kulima ekari 26,500 za kahawa, ekari 12,500 za umwagiliaji za mpunga na ekari 400 za mkonge na korosho. Miche 3,000 imeandaliwa na kulima michikichi huko  Burombola katika ekari 2,000.

Kutokana za uzalishaji huo, Suma JKT ilichangia jeshi Sh bilioni 1.5 na hivyo jeshi likafaulu kununua matrekta 15 na mashine nyingine za kuzalishia.

JOPO la Majaji 12 nchini Marekani limemtia hatiani ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi