loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mamelodi yaipiga Belouzidad mkono

TIMU ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini imeibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya wenyeji wao CR Belouzidad ya Libya katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam jana.

Katika mchezo huu ambao Mamelodi walitawala kwa dakika zote 90, ilishuhudiwa mshambuliaji wa timu hiyo, Thenba Zwane akiibuka nyota wa mchezo huo baada ya kufunga mabao mawili, huku Shalulile Maboe na Roméo wakiifungia timu hiyo mabao mengine.

Licha ya CR Belouzidad mchezaji wao mmoja kutolewa nje kwa kadi nyekundu mwanzoni mwa kipindi cha kwanza, lakini kilichowaponza wenyeji hao wa mchezo huo ni kutaka kuwashambulia wapinzani wao Sundowns ilhali wapo pungufu. 

Kwa ushindi huo, Mamelodi Sundowns imefikisha pointi sita na kukaa kileleni mwa kundi B, ikifuatiwa na TP Mazembe iliyo na pointi, mbili huku  CR Belouzidad ikishika nafasi ya tatu kwa kukusanya pointi moja sawa na Al Hilal ya Sudan.

Mechi hiyo imechezwa Dar es Salaam baada ya CR Belouzidad kuomba kutumia uwanja wa Mkapa kama uwanja wake wa nyumbani kwenye michuano hiyo kutokana na tishio la virusi vya corona nchini kwao.

MSHAMBULIAJI wa Simba, Meddie Kagere, anamhofia ...

foto
Mwandishi: Mohamed Akida

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi