loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ufisadi uliofanyika hospitali za rufaa haukubaliki

KAMATI iliyoundwa na serikali kuchunguza hospitali 28 za rufaa za mikoa, imebaini kuwepo viashiria vya hujuma, wizi na udokozi wa dawa na vifaa tiba, vyote vikiwa na thamani ya Sh bilioni 26.7.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Dorothy Gwajima amemuagiza Katibu Mkuu Afya, Profesa Mabula Mchembe afanye mabadiliko ya viongozi katika hospitali zote 28 kulingana na nafasi ya kila kiongozi alivyoshiriki kusababisha hasara hiyo.

Kwa mujibu wa Dk Gwajima, Februari Mosi mwaka huu, wizara iliunda kamati ya watalaamu kutoka wizara na taasisi za sekta mbalimbali, kufuatilia katika hospitali hizo kwa kipindi cha miezi 18 kuanzia Julai 2019 hadi Desemba, 2020.

Alisema kamati hiyo ilitaka kubaini changamoto za upatikanaji duni wa dawa na vipimo licha ya kuongezeka fedha za dawa. Alisema jumla ya dawa na vipimo 25 hadi 20, vilifuatiliwa kuanzia ununuzi, mapokezi na matumizi.

Kamati ilibaini upungufu mkubwa kwenye usimamizi wa dawa hizo katika hospitali za rufaa. “Kwa mujibu wa matokeo haya ni dhahiri kuwa huu ni usimamizi dhaifu wa mifumo ya udhibiti wa mali ya umma, dalili za hujuma, wizi na uwajibikaji usiofaa wa baadhi ya viongozi katika ngazi zote za uongozi hadi kwa mtumishi mmoja mmoja,” amesema Dk Gwajima juzi alipotangaza matokeo ya kamati ya uchunguzi.

Itakumbukwa kuwa uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli ulipoingia madarakani, uliongeza bajeti ya dawa kutoka Sh bilioni 31 mwaka 2015/16 hadi kufikia Sh bilioni 270, hivyo matarajio ni kuwa dawa zitakuwa za kutosha hospitalini na Watanzania watapata tiba nzuri kutokana na uboreshaji huo mkubwa.

Hivyo kunapoibuka dalili za hujuma na wizi katika matumizi ya dawa, siyo tu zinakatisha tamaa, bali zinarudisha nyuma nia nzuri ya serikali ya kuhakikisha Watanzania wanapata dawa na tiba nzuri wanapokwenda kutibiwa.

Ndio maana tunaunga mkono uamuzi wa Dk Gwajima wa kuagiza kufanyika mabadiliko ya viongozi katika hospitali hizo na pia kuchukuliwa kwa hatua za kinidhamu kwa watumishi watakapobainika kwenda kinyume cha sheria, kanuni na taratibu za ununi na ugavi wa bidhaa za afya.

Lakini haitoshi tu kufanya mabadiliko hayo na kuchukua hatua za kinidhamu kwa mujibu wa utumishi wa umma, bali kuchukua hatua zaidi za kisheria kwa wote watakaobainika kuhusika katika ufisadi huu, ambao unatia doa kazi kubwa inayofanywa na serikali katika sekta ya afya kwa kuhakikisha kunakuwapo kwa dawa za kutosha hospitalin

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

1 Comments

  • avatar
    Omary Abdallah
    11/04/2021

    Duuh hatari sana

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi