loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tasaf yasaidia 10 wa kaya maskini kusoma vyuo vikuu

MFUKO  wa Maendeleo ya Jamii(TASAF) wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, umefanikiwa kuwawezesha wanafunzi 10 walioko katika  kaya masikini kupata mkopo wa kusoma vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini .

Wanafunzi hao ambao wametoka katika familia zilizoko katika Mpango wa Kunusuru Kaya  masikini wamewezeshwa kupata mkopo huo kupitia barua za uthibitisho wa bodi ya mikopo kwa asilimia 100.

Hayo yamebainika jana wakati wa ziara ya watalaamu kutoka Tasaf iliyofanyika wilayani Maswa.

Ofisa ufuatiliaji Tasaf wilaya ya Maswa, Geace Tungaraza alisema katika sekta ya elimu wamewezesha wanafunzi elimu ya msingi na sekondari kupata mahitaji ya shule na wengine kupata mikopo vyuo vikuu.

Tungaraza alisema walengwa wengi wamenufaika kupitia ruzuku ya elimu kwani watoto wao wengi kwa sasa wanasoma na kufaulu vizuri kupitia ruzuku hiyo.

"Toka mpango wa kunusuru maskini uanze kutekeleza azma yake, walengwa wengi wamenufaika na mpango huo, mpaka sasa katika ruzuku ya elimu jumla ya wanafunzi 10 wamepata mikopo toka bodi ya mikopo chini ya udhamini wa Tasaf,"alisema.

Marry Masalu mlengwa na mwanakikundi wa Mwanzo Mgumu, alisema hapo awali maisha yao yalikuwa magumi kiasi hata kuchekwa na majirani zao lakini kupitia Tasaf wameweza kuheshimika na kubuni miradi ya kilimo na ufugaji.

Alisema miradi waliyobuni kupitia kikundi cha wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya maskini imewasaidia kusomesha watoto wao na kuendesha maisha yao ya kila siku.

foto
Mwandishi: Happy Mollel, Maswa

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi