loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ataka mkakati kuzuia ‘hitilafu’ ya maadili kwa vijana

WAZIRI wa Katiba na Sheria Dk Mwigulu Nchemba amewataka wadau wa haki za watoto nchini kuweka mkakati wa kuzuia mmomonyoko wa maadili kwa vijana.

"Tuwaze upya, tumefaulu kwa asilimia 100 katika kutetea haki za watoto nchini, lakini tumeshindwa kwa asilimia 100 katika kuwaandaa watoto ili waje kutoa mchango katika taifa," alisema jijini hapa jana.

Dk Mwigulu alisema hayo wakati akizindua Mpango Mkakati wa Pili wa Maboresho Endelevu ya Haki Mtoto (2020/21-2024/25).

Dk Mwigulu alisema sheria, kanuni na kampeni nyingi zimefanyika kwa ajili ya kulinda haki za watoto kwa asilimia 100, lakini watoto wamelemazwa kwa asilimia 100 kwa kukosa malezi bora.

Dk Mwigulu pia alimwagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Profesa Sifuni Mchome kuhakikisha Mpango Mkakati wa Pili wa Maboresho Endelevu ya Haki Mtoto nchini unatafsiriwa kwa Kiswahili ili ujumbe uifikie jamii kwa urahisi.

Alisema wizara itaendelea kufanya jitihada mbalimbali za kuratibu vyema mpango huo ikiwemo kuimarisha mfumo wa ulinzi wa mtoto, kuongeza uelewa wa haki za mtoto katika jamii, kufanyika kwa maboresho ya sera na sheria pamoja na kuimarisha uratibu wa ufuatiliaji wa utekelezaji wa mkakati.

Akizungumzia mafanikio yaliyotokana na Mpango Mkakati wa kwanza Dk Mwigulu alisema uliwezesha kuboreshwa kwa sheria mbalimbali zinazohusu mtoto ambapo moja ya sheria iliyorekebishwa ni ya dini inayosema kuingia katika mahusiano ya ndoa ni kosa la ubakaji.

"Nitoe rai kwa taasisi kujenga uelewa kwa jamii kuhusu haki na wajibu wao kwa mtoto mwaka 2015 ilitungwa Sheria kuhusu vitendo vya ukatili kwa mtoto, uanzishwaji wa madawati ya jinsia katika vituo vyote vya polisi pamoja na kufanikiwa huku hatutaishia hapa tuna wajibu wa kuwalinda na kuwaandaa wawe raia wema katika taifa letu na wasimame wenyewe katika maisha yao," alisema.

Kwa upande wake, Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto(UNICEF) nchini, Shalini Barugua aliipongeza Serikali kwa juhudi kubwa inazochukua kulinda haki za mtoto mijini na vijijini.

Awali akizungumza katika uzinduzi huo, Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Profesa Mchome alieleza baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo ikiwa ni  pamoja na uchache wa wataalamu wa masuala ya watoto, taasisi kutotenga bajeti, baadhi ya magereza kukosa sehemu maalumu  kwa ajili ya watoto.

JOPO la Majaji 12 nchini Marekani limemtia hatiani ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi