loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Lwaga hatamani Bongo Fleva

MSANII wa muziki wa Injili Joel Lwaga amesema hafikirii kuhamia katika muziki wa Bongo Fleva na wala hawazii kwasababu alipo ni mahali sahihi kwake.

Akizungumza Dar es Salaam nyota huyo anayefanya vizuri kwenye muziki huo, alisema anafurahia kile anachokifanya na ndicho kitu kinachompa amani katika maisha yake.

“Sijawahi kufikiria kuimba muziki mwingine kwasababu nafurahia kuimba Injili ingawa itaonekana muziki wa Bongo Fleva ndio wenye pesa nyingi, lakini hapa nilipo ndipo nilipoitiwa,”alisema.

Lwaga alisema yeye bado ni msanii mwenye ndoto na anatafuta nafasi ya kufanya makubwa zaidi siku zijazo.

Alisema kama pesa kwa sasa anapata kidogo na anaamini zitakuja nyingi baadaye kadiri muziki wake unavyozidi kukua.

Msanii huyo ni miongoni mwa nyota wa muziki wa Injili nyimbo zao zinakubalika kwa watu wengi bila kujali dini na wasanii wengi wa muziki wa kizazi kipya wamekuwa wakiomba kurudia nyimbo zake kutokana na kugusa hisia za wengi.

Baadhi ya nyimbo zake zilizofanya vizuri ni pamona na Sitabaki kama nilivyo, Mimi ni wa juu, Nafasi Nyingine, Wanitazama na Usipigane.

KLABU ya soka ya Simba imeingia mkataba ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi