loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wizara zaagizwa kurahisisha mfumo ‘Sema na Rais Mwinyi’

RAIS wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amezitaka wizara za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuviimarisha vitengo vyao vya habari ili kurahisisha utekelezaji wa kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi “Sema na Rais Mwinyi.

” Dk Mwinyi aliyasema hayo jana Ikulu jijini Unguja wakati alipokutana na uongozi wa Wizara ya Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi pamoja na watendaji wa ofisi hiyo, ikiwa ni mkutano kwa ajili ya kuripoti utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa Rais kwa mawaziri na makatibu wakuu wakati alipowaapisha.

Alieleza kwamba kuna haja ya kuhakikisha vitengo hivyo vya habari katika wizara za SMZ vinaimarishwa ili kuhakikisha malengo yaliokusudiwa ya mfumo huo yanafikiwa.

Katika mkutano huo ambao Makamu wa Pili wa Rais, Hemed Suleiman Abdalla alihudhuria, alieleza kuwa ni vyema pale wananchi watakapoanza kutoa malalamiko yao wakawa wanapata majibu kwa uhakika kutoka taasisi husika.

Alisisitiza haja ya kuwepo kwa mtu maalumu atakayehusika na kazi hiyo katika vitengo hivyo wizarani ambaye atakuwa anaripoti na kupeleka sehemu husika malalamiko hayo na hatimaye kupatikana majibu kwa haraka.

Katibu Mkuu Kiongozi, Zena Ahmed Said alieleza haja ya kuwepo elimu zaidi kwa wananchi kuhakikisha malengo ya mfumo wa “Sema na Rais Mwinyi” yanafikiwa.

JOPO la Majaji 12 nchini Marekani limemtia hatiani ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Zanzibar

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi