loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

UAE kuja kutembelea viwanda vya nyama

BALOZI wa Falme za Nchi za Kiarabu (UAE) nchini, Khalifa Almarzooqi Abdulrahman amesema ataandaa wajumbe kutoka falme hizo kuja nchini kutembelea viwanda vya kuchakata nyama ili kujiridhisha na ubora wa nyama kwa ajili ya kupeleka katika nchi zao.

Akizungumza na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki, baada ya kumtembelea jana Dar es Salaam, balozi huyo amesema ni muhimu kwa viwanda vya kuchakata nyama vilivyopo nchini kupata soko la uhakika katika Nchi za Falme za Kiarabu kwa kuzingatia Tanzania ni nchi ya pili kwa kuwa na idadi kubwa ya mifugo Afrika.

Aidha, amewaasa wamiliki wa viwanda hivyo kuketi pamoja na kuwa na umoja wao katika kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo ya kutafuta masoko ya bidhaa zao.

Kwa upande wake, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Ndaki amemweleza balozi huyo kuwa viwanda vingi vya kuchakata nyama vinakabiliwa na changamoto ya masoko kupeleka bidhaa zao nchi za nje kutokana na kudaiwa kukosa sifa kulingana na baadhi ya sheria na kanuni zilizopo katika nchi hizo za kuingiza nyama kutoka nchi za nje.

“Viwanda vyetu vya kuchakata nyama licha ya kuwa na uwezo mkubwa wa kuchinja idadi kubwa ya ng’ombe, mbuzi na kondoo, lakini bado vinakabiliwa na changamoto ya kukosa masoko ya kupeleka bidhaa zao mara baada ya kuchakata nyama,” alisema Ndaki.

Kuhusu ujumbe kutoka UAE kuja nchini kutembelea viwanda vya kuchakata nyama na kujiridhisha na ubora wa bidhaa zinazozalishwa kama alivyoahidi balozi wao, alisema ujumbe huo utakuwa ni mwanzo mzuri wa viwanda hivyo kupata masoko ya bidhaa zao nchi za nje.

JOPO la Majaji 12 nchini Marekani limemtia hatiani ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi