loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tanesco yaomba radhi katikakatika ya umeme

SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco) limeomba radhi Watanzania kwa mwenendo wa kukatikakatika kwa umeme unaoendelea sasa na kusema kumesababishwa na matengenezo makubwa ya mitambo mbalimbali ya kufua umeme inayofanyiwa kazi na kuahidi tatizo hilo litaisha ndani ya wiki moja kuanzia sasa.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Dk Tito Mwinuka jana alipokuwa akizungumzia hali ya umeme nchini na kusema wamepokea maelekezo ya Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani aliyoyatoa juzi jijini Dar es Salaam alipofanya ziara kwenye mitambo ya kufua umeme wa gesi ya Kampuni ya Songas.

Dk Mwinuka alisema hali ya umeme kwa sasa katika maeneo tofauti nchini imekuwa ya kukatikakatika na kuleta usumbufu kwa wananchi na hiyo imetokana na matengenezo hayo makubwa ya mitambo hiyo yaliyoanza Februari 25, mwaka huu na yanatarajiwa kukamilika siku chache kuanzia sasa.

“Tunawaomba sana radhi Watanzania kwa hali ya umeme ya kukatikakatika, imesababishwa na matengenezo makubwa ya mitambo ya kufua umeme, ila ndani ya kama wiki kuanzia sasa hali itatengemaa,” alisema Dk Mwinuka.

Alitoa mwito kwa mafundi wanaoendelea na kazi hiyo kuhakikisha wanafanya kazi hiyo kwa weledi kwenye mitambo hiyo ambayo ni pamoja na ya Tanesco ili kurejesha huduma.

“Kituo cha Songas kinachozalisha umeme megawati 180 kwa sasa kinapata gesi pungufu ya kuzalisha umeme ila wanatumia bomba la TPDC la gesi kuzalisha umeme megawati 115, badala ya 180 hivyo baadhi ya maeneo yanakosa umeme, ila tatizo litaisha muda mfupi,” alisema mtendaji huyo wa Tanesco.

Alisema mitambo inayofanyiwa matengenezo ni pamoja na ya Tanesco katika vituo vya kuzalisha umeme wa maji, mitambo ya Kampuni ya Songas inayofua umeme wa gesi ya Songosongo, na mitambo ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) inayofua umeme wa gesi asilia.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Songas, Anael Samuel alisema matengenezo ya mitambo yao imefikia muda wake kwa mujibu wa taratibu za mitambo hiyo na waliafikiana na wadau wao Tanesco na TPDC kufanya kazi hiyo.

JOPO la Majaji 12 nchini Marekani limemtia hatiani ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi