loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Simba yawafuata El Merreikh

KIKOSI cha Simba cha wachezaji 25 kilitarajiwa kuwasili Sudan jana kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya El Merreikh utakaochezwa Jumamosi.

Simba imekwenda huko kutafuta rekodi nyingine ya kupambana na kushinda ugenini ikiwa inaongoza Kundi A kwa pointi sita baada ya kushinda michezo miwili.

Kikosi kilichokwenda ni Aishi Manula, Beno Kakolanya, Ally Juma, Shomari Kapombe, Joash Onyango, Pascal Wawa, Erasto Nyoni, Gadiel Michael, Mohamed Hussein, Jonas Mkude, Rally Bwalya, Mzamiru Yassin na Luis Miqquisone.

Wengine ni Hassan Dilunga, Ibrahim Ajibu, Clatous Chama, Francis Kahata, Meddie Kagere, John Bocco, Miraji Athumani, Chris Mugalu, Peter Muduhwa, Tadeo Lwaga, Kennedy Juma na David Kameta.

Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes alisema mchezo huo unaweza kuwa mgumu kwa kuwa wenyeji hawatakubali kupoteza mchezo wa tatu mfululizo.

MSHAMBULIAJI wa Simba, Meddie Kagere, anamhofia ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi