loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Dk Abbas awashukia watendaji BMT

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Hassan Abbas amewataka watendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kufanyakazi kwa bidii na wale watakaoshindwa wataondolewa.

Dk Abbas aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam alipofanya vikao vya kukagua utekelezaji wa kazi na maagizo ya viongozi kwa baraza hilo pamoja na Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (Cosota).

Katibu Mkuu huyo aliongeza kuwa kuna baadhi ya hatua zimeanza kuchukuliwa kutokana na utendaji mbovu, akiwemo aliyekuwa Kaimu Msajili wa Vyama vya Michezo.

“Mtendaji Mkuu pendekeza ndani ya siku saba mtu mwingine wa kukaimu nafasi hiyo ulete wizarani, huyu msajili aliyekuwepo hapa amesharejeshwa kwenye majukumu ya taaluma yake.”alisisitiza Dk Abbas.

Aidha, Dk Abbasi alitumia kikao hicho na BMT kuonya baadhi ya watendaji akiwemo mmoja wa watumishi wa Idara ya Utawala katika baraza hilo kubadilika la sivyo atabadilishwa.

“Wizara inapokea malalamiko mengi kuhusu utendaji wako sasa inawezekana ni majungu au kweli una tatizo.

Kazi ya Idara ya Utawala ni kufanikisha mambo sio kukwaza watumishi na kuwatengenezea jakamoyo.

Sasa leo nilikuwa niondoke na wewe, lakini ngoja tukupe muda kukuangalia zaid, “alisema Dk Abbas.

Hata hivyo, awali Dk Abbas alizungumza na Menejimenti ya Cosota, ambapo alisisitiza watendaji hao kukamilisha maboresho ya mifumo yanayoendelea, ili wasanii na wabunifu wengine waanze kupata migao yao.

“Wizara ikiongozwa na Waziri wetu Innocent Bashungwa na Naibu wake Abdallah Ulega kwa sasa katika nguzo muhimu za mageuzi katika sekta zetu nne tumekubaliana hili la utawala bora kuanzia Wizarani, kwenye Taasisi na hadi kwenye asasi za wadau wetu ni muhimu na tutalisimamia ipasavyo.

Zama za uzembe, majungu, mizungu na watu kuwekeza katika fitna na akadabraha zimekwisha. Tunanyoosha mambo, kila mtu alipo anyooke kabisa kabla hatujafika kumnyoosha.”

JOPO la Majaji 12 nchini Marekani limemtia hatiani ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi