loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Prof Muhongo kuwafikia wananchi kwa urahisi

Mbunge wa Musoma Vijijini, Prof  Sospiter Muhongo ameanzisha utaratibu wa kupita nyumba hadi nyumba na maneno ya kazi ili kusikikiza kero za wananchi wa jimbo la musoma vijijini mkoani mara.

Katika kutekeleza adhma hiyo, Prof Muhongo aligawa pikipiki sita kwa wasaidizi wake ili ziwasaidie  kutekeleza mpango huo kwa urahisi.

Muhongo aliwapangia wasaidizi wake maeneo ya kazi ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini na kuwataka kukabidhi ripoti zao kila jumamosi kwa mbunge huyo.

Aidha, ameToa vitendea kazi ikiwa ni pamoja na simu janja ‘Smartphone’ sambamba na vifurushi vya internet, Kompyuta mpakato ‘Laptop’ na vifaa vinavyopima na kutambua eneo  ‘GPS.

Jimbo la Musoma Vijijini lina kata 21 zenye vijiji 68 na vitongoji 374.

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi